Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS MAGUFULI KUUNGURUMA MKUTANO WA HADHARA JUMAPILI KAHAMA


Rais John Magufuli anatarajia kufanya ziara wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambako atafanya mkutano wa hadhara kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliopita. 

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu alisema jana kwamba Rais Magufuli atawasili hapa Jumamosi jioni kabla ya kufanya mkutano wa hadhara Jumapili. 

Nkulu aliwataka wananchi wa Kahama na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kumlaki kiongozi huyo katika ziara hiyo ambayo alisema: “Lengo lake ni kuwapongeza wananchi wa Kahama kwa kumpa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliomalizika mwaka jana.” 

Alisema ziara hiyo ni muhimu kwa kuwa ni ya kwanza mkoani Shinyanga akianzia na Kahama. 

“Tujipongeze wananchi kutokana na kupata bahati ya wilaya chache zilizotembelewa na kiongozi huyu, Kahama imekuwa mojawapo,” alisema Nkulu. 

Alisema kwa kuwa Jumamosi ni siku ya usafi kitaifa, kila mmoja wilayani humo ahakikishe anaweka mazingira katika hali ya usafi na kuwaonya wafanyabiashara kuwa atakayeshindwa kufanya hivyo hataruhusiwa kufungua biashara. 

“Nitafanya ukaguzi Jumamosi kuhakikisha kila mtu anashiriki usafi. Hilo ni agizo la kitaifa kwa sasa lazima kila mmoja awajibike, nimewaagiza watendaji wote wa kata kusimamia hilo,” alisema Nkulu. 

Alisema wananchi watatangaziwa ratiba yote ya Rais Magufuli kwenye gari la matangazo ambalo litazunguka mji mzima wa Kahama kuwaeleza muda na eneo ambalo kiongozi huyo atafanyia mkutano.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top