Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UBUYU MPYAAA.... FLORAH MBASHA AMWANGUKIA MUMEWE MBASHA

Habari ya mjini ni Mwimba Injili Bongo, Flora Mbasha kudaiwa kumwangukia mumewe waliyetengana, Emmanuel Mbasha kwa kumuomba radhi ndoa yao ichipuke upya kama zamani.
ema-mbashaEmmanuel Mbasha
Kwa mujibu wa mtoa ubuyu ambaye ni muumini wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT) ‘Mito ya Baraka’, Kariakoo, Dar linaloongozwa na mchungaji Bruno Mwakibolwa, ambalo zamani wawili hao walikuwa wakisali, baada ya jitihada za kurudiana kugonga mwamba, Flora alimfuata mchungaji ili aweze kumsaidia arudiane na mumewe.“Iko hivi, Flora awali alikuwa mzito kuomba radhi lakini hivi karibuni aliamua kujisalimisha pale kanisani EAGT, akakutana na mchungaji, akamuelezea matatizo yake.

MBASHA3.jpg“Mchungaji alimwambia atalifanyia kazi suala hilo. Akamuita Mbasha (Emmanuel), akamhoji kwa saa tatu, lakini hoja alizozitoa Mbasha, mchungaji mwenyewe alinyoosha mikono na kumwambia awe huru,” alisema mtoa ubuyu huyo akiomba hifadhi ya jina lake.
“Mbasha alifunguka sana. Alimueleza kuwa, Flora alifikia hatua ya kutamka kuwa mchungaji wake ni Gwajima. Sasa iweje leo amuone Mwakibolwa?

“Pia Ima alimueleza mchungaji kuwa, Flora alizaa mtoto na mwanaume mwingine wakati yeye ana matatizo. Flora huyohuyo alikomaa kuhakikisha yeye anafungwa kwa kusimamia ile kesi ya ubakaji.
“Lakini pia, mara baada ya Mbasha kushinda kesi, Flora alienda kukata rufaa japo alishindwa kwa kuchelewa muda wa kukata rufaa. Kwa hoja hizo, mchungaji akaona hakuna jinsi zaidi ya kila mtu kuishi kivyake,” alisema mtoa taarifa huyo.

Nje ya kanisa hilo juzi, paparazi wetu alikutana na mmoja wa waumini aliyesema anaitwa Masasi ambaye alikiri Flora kufika kanisani hapo kuongea na mchungaji lakini alidai hajui maongezi yao yalihusu nini.

Jitihada za kumpata mchungaji Mwakibolwa ziligonga mwamba kwa kuambiwa alikuwa bize na majukumu ya huduma ya Bwana.

Alipotafutwa Flora ili aweze kuzungumzia suala hilo, simu yake haikupatikana hewani lakini paparazi  wetu alifanikiwa kumpata Mbasha ambapo alipoelezwa ‘full’ stori, majibu yake yalikuwa hivi:

“Nyie mmeipata hiyo? Aisee nyie kiboko, mko makini na matukio. Labda mimi niseme tu hayo yalishapita, sipendi kuyazungumzia kwa sasa maana nilishayasahau. Kwa sasa mimi namshukuru Mungu naendelea vizuri na akipenda nitapata mwenzangu na nitawajulisha.”
Mwaka 2014, wawili hao walimwagana lakini miezi michache mbele, Mbasha alipata kesi ya kudaiwa kumbaka shemejiye mwenye miaka 17.

Uhasama wao ulizidi, ikadaiwa Flora alikuwa nyuma ya kesi hiyo. Mwaka jana, Mahakama ya Wilaya Ilala, ilimwona Mbasha hana hatia hivyo kuwa huru na kila mmoja kuishi maisha yake huku Flora akisali Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa mchungaji Josephat Gwajima na Mbasha akisali Mito ya Baraka.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top