Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAREKANI YAIPATIA TANZANIA BILIONI 895 KUFIKIA MALENGO

Serikali ya Marekani, kupitia shirika lake la Misaada ya Maendeleo USAID, imeipatia Tanzania msaada wa dola Milioni 407 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 895 zitakazotumika kwaajili ya kuendeleza sekta za Kilimo, Afya, Nishati ya Umeme, Elimu na Utawala Bora, katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia mwaka 2016/2020.

Hati za makubaliano hayo zimetiwa saini Jijini Dar es salaam, kati ya Mkurugenzi wa Shirika la USAID, Bi. Sharon Cromer, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.

Msaada huo ni sehemu ya dola milioni 800, sawa na zaidi ya shilingi trilion 1.76 ambazo serikali ya Marekani kupitia USAID, imepanga kuipatia Tanzania ili kufanikisha Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa katika kipindi cha miaka mitano ijayo, wenye lengo la kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Kiasi hicho cha fedha kitatumika na serikali ya Tanzania kupitia mfuko mkuu moja kwa moja wakati kiasi kingine kitatumiwa na Taasisi zisizokuwa za kiserikali zinazofanya shughuli zake hapa nchini kufanikisha malengo ya msaada huo.

Miradi iliyopewa kipaumbele ni pamoja na kupambana na UKIMWI na kifua kikuu, uzazi wa mpango, kupunguza vifo vya mama na mtoto, kukuza utawala wa kidemokrasia, usimamizi wa rasilimali za taifa, na kuwekeza kwenye sekta ya umeme ili kuimarisha sekta ya viwanda na uzalishaji mali.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top