Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Bashe awaponda wabunge walalamishi

Mbunge wa Nzega mjini, Hussein Bashe, amewataka wabunge kutimiza wajibu wao na sio kulalamika wakati wanalipwa kwa fedha za walipa kodi.

Mbunge huyo amezungumza hayo wakati akichangia muswada wa sheria ya upataji wa taarifa wa mwaka 2016. Bashe aliwataka wabunge wote kuungana kutimiza wajibu wa kisheria katika kutimiza majukumu yao ya kusimamia sheria na sio kulalamika mara kwa mara.

“Nataka niseme pale ambapo sisi wabunge tunakuja bungeni, tunalipwa na nchi hii,kwa kodi za watu maskini, kuja kuisimamia serikali, na sisi tunalalamika kuwa serikali imevunja katiba, imevunja sheria, it is our duty, kuisimamia serikali tuunganeni tufanye kazi yetu, kuisimamia serikali ifanye wajibu wake,” alisema Bashe.

“Sio fair kwa nyinyi kulalamika, je kwa wale waliotupigia kura?” alihoji. Nayasema haya kwasababu sisi sote ni waathirika wa kila jambo, pale ambapo tunataka kujivua responsibility na kutaka kuonyesha kwamba responsibility hii na madhambi haya ni ya wabunge wa CCM tu, it is your duty also kusimamia serikali hii,” alisisitiza.

“Mimi nataka niseme kwamba tusisuse ni ya kwetu sote it’s our duty kuungana kutafuta haki kwa yale tunayoamini ni ya wananchi wetu.”
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top