Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Jipu limeiva, linatakiwa kutumbuliwa Tanesco Magomeni

Jana usiku mida ya saa 1 usiku tulipata hitlafu ya umeme katika nguzo iliopo juu ya bati ambayo ndio inapokea umeme kuingiza ndani ya nyumba yetu. Hali haikuwa nzuri kabisa kwani shoti ilikuwa kubwa sana na ilidumu kuwa muda mrefu, ndipo tukatafuta namba ya Tanesco Magomeni na kuwapigia simu kuwa kunashoti ambayo inaweza kupelekea kuunguza nyumba tukajibiwa kuwa watu wa Emergency wanakuja tukawa tunasubiri huku shoti ikiendelea mara hali inatulia mara inazuka tena.

Lakini chakushangaza Tanesco hawakutokea na ukipiga simu unajibiwa kuwa wapo njiani wanakuja, masaa yanakatika muda na unakwenda tukipiga tena simu tunajibiwa wanakuja wapo njiani.

Kiukweli hili swala ni sugu kitengo cha Emergency Magomeni ni SHIDAAAAA'' yani hawana habari na kazi yao wala hawajali kabisa alafu zaraumbele pesa mbele yani wao ndio wao wanavyo taka wao ndivyo itakavyo kuwa.

Kila mtu analalamika na Kitengo hichi cha Emergency hawafanyi kazi sijui wanalala makwao sijui wamechoka kufanya kazi !!!!

Nyumba zinakaa giza mpaka siku 4 - 5 Tanesco hawajatokea na kila wakipigiwa simu jibu wapo njiani wanakuja, Hapa sibure kuna Jipu tena Kijipu uchungu kinatakiwa kutumbuliwa tu.

Tunaomba Uongozi wa Tanesco Makao Makuu walifanyie kazi hili swala kwani watu washachoka na hawa jamaa Emergency a,k,a wapiga Dili hawapo kikazi bali wapo kimasilahi tu wakipigiwa simu Kunatatizo kwenye Mahoteli wanakwenda kwasababu wanapewa pesa na wakipigiwa simu kwenye myumba za makazi hawaji kabisa.

Ni aibu kubwa sana kwa Tawi la Tanesco Magomeni kuwa na kitengo kama hichi ambacho kipo kimasilahi zaidi kuliko kutoa huduma kwa jamii.

Ni aibu kubwa kwa Mkuu wa Kitengo hichi cha Emergency ambae ni dhahiri kuwa kashindwa kazi kwa 100%

Ni aibu kwa Viongozi wote wa Tanesco Magomeni kushindwa kusimamia vizuri maswala madogo madogo kama hayo ya Nyumba kukosa Umeme kwa siku 4 -5 bila kurekebishiwa tatizo lililopo AIBUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU...
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top