Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mashine ya MRI yaanza kufanya kazi Muhimbili

 Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa wakati Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akieleza jambo kwa waandishi wa habari leo.

 Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya mashine ya MRI kuanza kufanya kazi. Kutoka kulia ni Mtaalamu wa MRI (MRI Technologist), Joshua Job na Daktari Bingwa wa Mionzi, Mussa Ndukeki wa hospitali hiyo

 Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano uliofanyika leo kwenye hospitali hiyo.

Mtaalamu wa MRI (MRI Technologist), Medadi Mallaya akimuhudumia mgonjwa leo.

Dar es Salaam, Tanzania. Mashine ya MRI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepona baada ya kuharibiika tarehe 24/08/2016. Mashine hiyo iliharibiika baada ya kutokea hitilafu ya umeme. Tangu mashine hiyo imepona tayari wagonjwa 52 wamepatiwa kipimo cha MRI. 

Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dk Flora Lwakatare amesema baada ya mashine hiyo kuharibiika, mafundi wa Philips kwa kushirikiana na mafundi wa Muhimbili walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hiyo. 
“Tarehe 26/08/2016, mafundi walibadilisha betri zote 31 na kufunga mpya ili kuongeza ufanisi katika mashine hii kwa kuwa betri za awali zilikuwa zimefungwa muda mrefu. Tarehe 28/08/2016 mafundi walibaini kwamba kifaa cha Gradient Module kilikuwa kimeharibiika na tayari hospitali kwa kushirikiana na Philips wameagiza kifaa hicho kutoka Uholanzi,” amesema Dk Lwakatare. 

Mmoja wa ndugu wa wagonjwa, Lazaro James, mkazi wa Singida amesema kwamba tangu kuharibiika kwa mashine ya MRI alikuwa akiisubiri na kwamba amefurahi baada ya kurejea kwa huduma hiyo. “Tunashukuru huduma za MRI zimerejea hapa Muhimbili, gharama zake ni nafuu kuliko kuliko kupata matibabu nje. Jambo lingine napenda kuwapongeza madaktari na wauguzi kwa utendaji bora. 


Naye Hawa Hussein mkazi wa jijini Dar es Salaam, ameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuwa imekuwa ikitoa huduma bora kwa wagonjwa. Hawa ameuopongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kufanya juhudi za kuiwezesha mashine hiyo kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa. Amesema kwamba madaktari wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii hivyo wana imani wataendelea kupata huduma bora na kwa wakati.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top