Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MFUMUKO WA BEI WAZIDI KUSHUKA

Kasi ya kupanda kwa bei za bidhaa na huduma imeanza kupungua nchini Tanzania kutokana na kiwango cha mfumuko wa bei unaopimwa kwa kigezo cha mwaka kupungua na kufikia asilimia 4.9 kutoka kiwango cha asilimia 5.1 kilichokwepo mwezi uliopita.

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraim Kwesigabo, amesema hayo leo na kutaja sababu zilizochangia kupungua kwa kasi hiyo ya bei ya bidhaa na gharama kuwa ni kushuka kwa bidhaa takribani zote, za vyakula na zisizo za vyakula.

Kwa mujibu wa Bw. Kwesigabo, hali hiyo imeifanya thamani ya shilingi katika manunuzi kuimarika kiasi ambapo kila shilingi mia moja inaweza kufanya manunuzi yenye thamani ya shilingi 96 na kwamba kiwango cha sasa cha mfumuko wa bei hakina tofauti sana na ilivyo nchi nyingine za Afrika Mashariki isipokuwa Kenya tu ambako mfumuko umefikia asilimia 6.26.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top