Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MWENYEKITI ATUHUMIWA KUMMWAGIA TINDIKALI KATIBU

Geita. Polisi mkoani Geita, inamshikilia Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyantorotoro A, Gervas Kaiyelelo kwa tuhuma za kummwagia tindikali Katibu wa CCM Tawi La Nyantorotoro, Kulwa Kazinga kwa kile kinachodaiwa ni uhasama wa kisiasa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi alisema tukio hilo lilitokea Agosti 31 usiku, wakati katibu huyo akielekea nyumbani kwake. Kapufi alisema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha tukio hilo ni uhasama wa kisiasa baina ya mwenyekiti huyo ambaye ni wa Chadema na katibu wa CCM.

Akizungumza kwa shida kutokana na majeraha aliyoyapata ikiwamo kuungua maeneo ya uso na kifuani, Kazinga alisema siku hiyo akiwa na jirani yake aliyemtaja kwa jina la Selestine Misungwi wakitokea makao makuu ya kata hiyo, alitokea mtu msituni na kummwagia majimaji ambayo  yalianza kumuwasha na alihisi maumivu makali.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top