Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ndege ya Air Tanzania kuwasili nchini wiki ijayo
Moja kati ya ndege mbili zilizonunuliwa na serikali kuimarisha usafiri wa anga nchini, inatarajiwa kuwasili Jumanne wiki ijayo.

Kauli hiyo imetolewa na naibu spika wa bunge, Dk Tulia Ackson, wakati akitoa taarifa ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Pro Makame Mbarawa.

“Waziri Mbarawa ameniarifu kuwa, ndege hiyo itatua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere “,alisema Dk Tulia.

“Pia natoa wito kwa wabunge na viongozi kushiriki kuipokea ndege hiyo aina ya Dash 8-Q400 yenye uwezo wa kubeba abiria 76,”aliongeza.

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, imedhamiria kurejesha fahari ya sekta hiyo nchini kwa kuchukua hatua kadhaa, ikiwamo ya kununua ndege na kuboresha viwanja vya ndege nchini. Lengo ni kuhakikisha kuwa kila mkoa unakuwa na kiwanja cha ndege cha kisasa, chenye ubora unaofaa kutua ndege
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top