Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ndoa ya Shamsa na siri ya gauni la kijani

Hujashtukia kuwa mastaa wa kike waliofunga ndoa hivi karibuni walivaa gauni la kijani. Sahau kuhusu Wastara na Flora Mvungi ambao walivaa pinki na nyekundu.

Unaikumbuka harusi ya Mwana FA, Mr Blue, Shamsa Ford na Riyama Ally? Mabibi harusi walivaa gauni la kijani. Labda na wewe ulijiuliza kwa nini imekuwa hivyo, je, ni fasheni.

Mwigizaji Shamsa Ford anaizungumzia rangi hiyo kwa kusema ndiyo anayoipenda, lakini alipouliza wakubwa avae nguo ya rangi gani siku ya ndoa walimshauri kuvaa rangi hiyo.

“Niliambiwa ni rangi bora kuvaliwa na mtoto wa Kiislamu siku ya kuivaa siku ya ndoa yake, ”anasema Shamsa.

Kwa upande wa mwigizaji Riyama Ally anasema kuwa tangu makuzi yake amekuwa anasikia sifa za rangi hiyo, hususani siku ya ndoa kuwa ina baraka.

Anasema; “Nafahamu ni rangi yenye baraka na inayopendwa, niliwahi kusikia kuna hadithi kama siyo aya za kitabu kitukufu Msahafu zikiisifu rangi hiyo ikiwamo kuwataja watakaovaa kuwa ni wateule.

“Nimekuwa nikiamini hivyo na Waislamu wengi huamini hilo na ndoa nyingi za Kiislamu bibi harusi huvaa rangi hiyo,” anasema Riyama.

Ipo katika imani

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum anaizungumzia rangi hiyo katika dini kuwa ni miongoni mwa rangi bora ukiitoa rangi nyeupe.

Anasema kuna aya kadhaa zimeitaja rangi hiyo kuwa ni bora, ikiwamo kutajwa kwenye Qur-aan kuwa ni nguo ambazo watakazozivaa watu wa peponi.

Anafafanua kuwa mbali ya kuvaliwa na watu wa peponi hata Mtume Muhammad (SAW), alikuwa anapenda kuvaa kiremba cha rangi ya kijani na katika matukio maalumu alikuwa anavaa kabisa kanzu ya kijani.

“Unatajwa ubora wa rangi hiyo katika sura ya Al-Insaanna sura ya Al-Kahf, kuwa itavaliwa na watu wa peponi na kuwa ni rangi bora, ”anasema Alhad Mussa.

Ni rangi ya neema

Rangi ya kijani inatajwa kuwa imetulia na ni rangi ya asili, mara nyingi hii inahusishwa na mazingira.

Wapenda mazingira na watunzaji huithamini na kuiheshimu rangi hiyo.

Kizuri zaidi watu wanaodumisha asili huipenda rangi hiyo ikiwamo wanaofuga rasta, maarufu marasta hupenda kuvaa rangi hiyo.

Ukiachilia uthabiti wa rangi hiyo katika mifano hiyo michache, mabibi harusi wengi hupenda kuvaa rangi hiyo siku ya ndoa, ingawa mara chache kuwakuta ameivaa hiyo kwenye hafla ya kujipongeza kwa kupiga hatua hiyo muhimu ya kuwa mwili mmoja.

Mbali ya mastaa hao waliofunga ndoa mastaa wengine waliowahi kuvaa rangi hiyo katika hafla kubwa ni pamoja na Wema Sepetu na Kajala Masanja.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top