Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

NIDA yatoa vitambulisho vya Taifa vipya kwa Wabunge

  Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa jimbo la Musoma, Mhe.Profesa Sospeter Muhongo
akipokea Kitembulisho chake cha Taifa chenye saini kwa furaha kubwa kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Na Hifadhi Hati NIDA. Bi. Rose Mdami.
 Waziri wa Katiba na na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe, akiwa mwenye furaha kubwa baada ya kuchukua Kitambulisho chake kipya Bungeni Dodoma. NIDA imeanza kutoa vitambulisho vipya vyenye saini kwa viongozi wakiwemo Waheshimiwa Wabunge zoezi linaloedelea mkoani Dodoma sambamba na kikao cha Bunge.
 Deo Sanga, akieleza faida ambazo tayari ameshazipata kwa kutumia Kitambulisho chake cha Taifa. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi hati NIDA Bi, Rose Mdami. Mhe. Sanga amepokea kitambulisho chake leo katika Ofisi za Bunge Dodoma
 Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipata huduma kutoka kwa maafisa
wa NIDA ambao wapo bungeni hapo kutoa vitambulisho vipya kwa waheshimiwa wabunge Mjini Dodoma.
Mbunge wa Muheza na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya Bunge Mheshimiwa Adadi Rajabu akipokea kitambulisho chake kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati NIDA Bi. Rose Mdami katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top