Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Polisi waingilia kati sakata la kamata kamata 'gesti'

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam anatoa rai kwa wakazi wa Jiji la Dar Es salaam na wageni wanaoingia jijini wakitokea mikoani  kupuuza  taarifa za sauti  zinazozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Polisi wanawakamata ovyo watu wanaolala kwenye nyumba za kulala wageni.

Taarifa hizo za uvumi  zinazoendelea kuzagaa  kwenye mitandao ya Kijamii kama WHATSAPP, TELEGRAM na pia zimechapishwa kwenye baadhi ya magazeti kwamba Askari Polisi wanawakamata watu  ovyo mchana wakiwa kwenye nyumba za kulala wageni  kwa madai ya kukamata kwa makosa ya uzembe na uzururaji na pia kutimiza kauli ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ‘HAPA NI KAZI TU’.

Kimsingi niwatoe hofu raia wema kuwa tunaendelea na oparesheni za kuwasaka watuhumiwa wa makosa mbalimbali yakiwemo wanaofanya biashara ya nyumba za kulala wageni kinyume cha sheria (guest bubu), mjambazi na wahalifu wengine wa makosa mbalimbali.

 Aidha taarifa za kuaminika zimebaini kuwa baadhi ya nyumba za kulala wageni zimekuwa zikitumika kuhifadhi magenge ya wahalifu, dada poa na kaka poa, hivyo Jeshi la Polisi tunawajibika kufuatilia na kuwakamata wahalifu.

Niwajibu wa Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye nyumba za kulala wageni, Hoteli, migahawa, Vilabu vya vileo,  kumbi za starehe zinazokesha na zisizokesha na watakaobainika kuvunja sheria, hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa. Sheria ya Mwenendo ya makosa ya jinai kifungu cha 60(1) (sura ya 77 iliyofanyiwa marekebisho 2002) kinampa nguvu askari kufanya ukaguzi wa maeneo yote yaliyotajwa hapo juu na kumkamata mtu yeyote anayetiliwa shaka akienda kinyume na utaratibu wa biashara hizo.

Sambamba na hayo nawatahadharisha wafanyabiashara wote wa nyumba za kulala wageni wafuate taratibu za kupokea wageni kwa kuandika kwenye vitabu, kuandika namba za vitambulisho vyao na sehemu wanayotoka, na pale watakapomtilia mashaka mteja yeyete watoe taarifa kituo chochote cha polisi.

Pia wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wa nyumba kumi wanawajibika kuwatambua wageni wote wanaoingia kwenye himaya zao na kuwachukulia hatua stahiki ili kuimarisha usalama katika jiji letu la  Dar Es salaam.

DAR ES SALAAM BILA UHALIFU INAWEZEKANA, TUSHIRIKIANE KUISAFISHA JIJI LETU

S.N.SIRRO - CP
 KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top