Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Polisi yachunguza kuzagaa viungo vya Mtoto

VIUNGO vinavyodhaniwa kuwa ni vya mtoto mchanga vimeonekana kuzagaa katika mtaa wa Butengwa, Kata ya Ndembezi, Manispaa ya Shinyanga bila kufahamika ni nani aliyesababisha vizagae.

Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa mtaa huo, Juma Derefa alipokuwa akizungumza na gazeti hili.

Alisema kuwa saa 5:00 asubuhi jana waliona viungo vya mtoto mchanga vikiwa vimezagaa mtaani na kutoa taarifa. Derefa alisema baadhi ya viungo vilikuwa vimebebwa na mbwa na baada ya kuona hivyo, walifuatilia.

“Viungo hivyo vimeonekana mbali na makazi ya watu jirani wa kwenye mtaa wa Mwadui. Viongozi wake tumewashirikisha na hadi sasa hatujamtambua aliyefanya kitendo hicho cha kikatili cha kutupa au kutelekeza viungo hivyo,” alisema.

Alisema huenda wananchi wanafahamu nani aliyekuwa na mtoto au mjamzito na kufanya kitendo hicho.

“Ndio tumeanza uchunguzi kwa kushirikiana na Polisi,” alisema Derefa. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Elias Mwita, alithibitisha kupata taarifa ya tukio hilo na alisema kuwa wanachunguza suala hilo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top