Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli alivyopokea taarifa ya tetemeko la ardhi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amepokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Tetemeko hilo limetokea Kagera na mikoa jirani ya Mwanza, Geita na Kigoma.

Pamoja na kupokea taarifa hiyo Rais Magufuli amepokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki mbili (USD-200,000/-) sawa na shs 437 milioni kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

Pia amepokea taarifa ya mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

Katika taarifa yake  Majaliwa amesema tetemeko hilo limesababisha vifo vya watu 17, majeruhi 440, nyumba 2063 zimeanguka, nyumba 14,081 zipo katika hali hatarishi na nyumba 9,471 zimepata uharibifu mdogo, huku watu 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mchango wa fedha  cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) taslimu uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kusaidia waathirika watetemeko la ardhi mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kusoma taarifa kuhusu Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Boniface Muhia mara baada ya kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais  Uhuru Kenyatta  wa Kenya na kwa misaada mbalimbali ya mabati 4,000 na vifaa vya majumbani ikiwemo magodoro na mashuka ambayo inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka Kenya muda wowote kuanzia sasa. Katikati ni Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa fedha taslimu kutoka Uganda pamoja na taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top