Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli apongezwa utaratibu maafa ya tetemeko la ardhi



Joseph Martin, Nottingham  

WATANZANIA bado tuko katika masikitiko kufuatia maafa yaliyoletwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera na baadhi ya maeneo ya Kanda ya Ziwa. Tetemeko hilo tunaambiwa ni la kiwango cha skeli ya 5.7 ambayo ni kubwa.

Watu 17 wamefariki kutokana na tetemeko hilo, mamia wamejeruhiwa na maelfu ya nyumba ama zimebomoka au zimeharibika kwa namna tofauti. Mimi binafsi nina ndugu zangu ambao ni waathirika wa tukio hili na namshukuru Mungu kwa misaa waliyopata.

Nimefuatilia sana yanayotokea kule Kagera na naendelea kufuatilia kwa sababu jamaa zetu wa kule kwa kweli wanahitaji msaada wetu ingawa na wao pia wanapaswa kuchukua hatua zao na za jamaa zao wa karibu katika kujinasua na janga lililowafika.

Maoni yangu leo si ya kueleza tukio hilo wala kufafanua maafa yalivyowagusa ndugu, jamaa na marafiki zetu, bali kimsingi, nimeandika kufikisha ujumbe kwa Mhe Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Pombe Magufuli. Nitaeleza kwa nini Dkt. Magufuli anapaswa kupewa hongera zake katika hili.

Mosi, tufahamu kuwa hili ni janga  la asili na ni jambo ambalo wanasayansi wanasema halitabiriki na hakuna mtu anaweza kujua lini tetemeko la ardhi litatokea. Lakini hata tukijua, bado ni ngumu kuzuia athari zake hasa kwa makazi na miundombinu.

Lakini tangu kutokea kwa jambo hili, labda tofauti na ilivyopata kutokea katika majanga mengine nchini kama vile mafuriko ya Kilosa na majanga mengine ya tetemeko au mafuriko, kwa mara ya kwanza, na ikiwa haina uzoefu bado wa muda mrefu katika uongozi, Serikali ya Magufuli imetuunganisha na imetutendea haki sana kwa kiwango chake.

Mara tu baada ya tukio, Waziri Mkuu alifika Kagera kuwajulia hali waathirika, kushiriki mazishi ya umma ya waliofariki na kutoa maagizo kwa watendaji wake juu ya hatua za haraka za kufanywa.

Mara tu baada ya Waziri Mkuu kutoka Kagera, Rais Magufuli ambaye hata baadhi ya watendaji wake waandamizi walishakuwa mjini Lusaka, Zambia alikokuwa aende kwa ajili ya sherehe za kuapishwa Rais Lungu, naye aliahirisha safari hiyo.

Rais aliahirisha safari na kubaki Dar es Salaam kuratibu kwa karibu maafa hayo na namna ya kuwasaidia waathirika. Na mara moja tuliona athari za uwepo wake nchini ambapo ilifanyika harambee Ikulu ambapo watanzania tukahamasishwa kuchangia.

Serikali ikachukua hatua muhimu za mawasiliano na hamasa kwa wadau ikiwemo kutangaza akaunti ya maafa na namba za simu za sisi kuchangia. Akaunti hizi, tofauti na miaka ya nyuma zimesambazwa sana katika mitandao ya kijamii na hata nimeona matangazo katika magazeti na katika televisheni. Mkuu wa Mkoa wa Kagera anatoa taarifa za mara kwa mara pia.

Serikali pia kupitia taasisi na wizara mbalimbali pia imeendesha matukio mengine ya kuchangia waathirika, imeratibu nchi nyingine za kigeni na Balozi kupeleka misaada Kagera na misaasa hiyo imeanza kuwafikia waathirika.

Nafahamu kuwa Serikali haikuwa na wajibu wa moja kwa moja katika hili kwa kuwa haikusababisha, lakini juhudi hizi ni za kupongezwa sana na za kukumbukwa sana. Mzee Magufuli Mungu akutangulie.

Nnitumie fursa hii pia kuwasihi watanzania wenzangu, katika kuwasaidia wenzetu, kama tulivyoanza, kusiwe tena na siasa wala watu kutafuta upungufu na kukosoa. Kila mmoja wetu “ajiongeze” wanasema vijana wa  mjini.

Hata kwa ndugu zangu waathirika nao pia tujue sisi na jamaa zetu tuna jukumu la kwanza katika hili na tujitume kujinasua katika janga hilo, Serikali inaweza kuleta kidogo cha kuchangia au kutufuta machozi, au kurekebisha miundombinu ya umma lakini tusibaki watu wa kusubiri tukidhani ndio tutafanyiwa kila kitu.

Hakuna Serikalini duniani inayoweza kufanya kila kitu hasa yanapotokea majanga makubwa hata ziwe na uwezo vipi. Niliwahi kufika Marekani kwenye eneo la janga la Septemba 11 pale Manhttan, New York na kukuta hata baada ya miaka 10 eneo lile halikuwa limeweza kurejea katika hali yake ya awali.

Kuna eneo kule Japan baada ya maafa ya mafuriko nimepata kuvikuta vikiwa hadi leo haviko katika sura yake ya awali. Naamini hata ndugu zangu wa Kagera wajue hili, yapo mambo yanaweza kufanyika yakawa bora zaidi kwa jitihada zao na za Serikali, lakini pia yapo yanayoweza kuchukua muda zaidi na au hata yasirejee katika hatua kama za awali.

Nihitimishe, hongera kwa JPM lakini pia Serikali na wadau wengine tuendeleze moyo huu huu na ushirikiano huu huu katika matukio mengine mengi zaidi yawe ya maafa au ya kawaida. Kama tulivyoungana katika suala la madawati na hili la maafa, naamini tukiendelea kuungana pamoja, Tanzania itasonga mbele.

Nawashukuru sana.

*Mwandishi wa makala haya amejitambulisha kuwa Mtanzania anayesoma Chuo Kikuu cha Nottingham, Uingereza.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top