Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS MAGUFULI 'AWAPAISHA' MAKONDA NA HAPIRais Magufuli akunwa barabara na utendaji kazi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe.Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Hapi alipofanya ziara ya Wilayani Kinondoni asubuhi ya leo.

Katika ziara hiyo Mhe Rais  Magufuli ameahidi kuwajengea nyumba wakazi 644 wa Magomeni Kota ambao waliobomolewa  makazi yao  na serikali ya manispaa tangu mwaka 2012.

Rais Magufuli aliendelea kusema Wananchi hao 644 watakaa kwenye nyumba hizo za ghorofa kwa muda wa miaka mitano bure/bila malipo kisha atawafanyia utaratibu wa kuwauzia ili ziwe chini ya himaya zao.

Mhe Magufuli alihitimisha ziara hiyo kwa kuwafagilia DC Hapi na RC Makonda kwa kusema kuwa ni vijana hodari na wachapakazi wanaomuwakilisha vema pia Mhe. Rais amewaasa wasikatishwe tamaa wasonge mbele, wote wanaowakatisha tamaa ipo siku watawaheshimu tu aidha alimpongeza Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kutekeleza agizo lake kwa wakati
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top