Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SERIKALI YALIPA BILIONI 500 ZA MADENI YA WASTAAFU

Waajiri nchini Tanzania wametakiwa kuwasilisha nyaraka za wastaafu katika kipindi cha miezi mitatu ili malipo ya wazee yaweze kuandaliwa kwa wakati.

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji na kueleza kuwa kucheleweshwa kwa malipo ya wastaafu kunatokana na waajiri kutowasilisha taarifa mapema na kuwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Agosti 2016 serikali imefanikiwa kulipa jumla ya shilingi bilioni 511.86 ikiwa ni malimbikizo ya mwajiri kwa watumishi waliostaafu.

Amesema katika fedha hizo jumla ya shilingi bilioni 83.25 zimelipwa ikiwa ni malipo ya deni kabla ya mwaka 1999, pamoja na kiasi cha shilingi bilioni 117 mafao ya pensheni za mwezi.

Dkt. Ashatu Kijaji ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Mjini Mary Chatanda aliyehoji kuhusu changamoto inayowakabili wastaafu ya kucheleweshewa mafao yao na mfuko wa pensheni wa PSPF katika mwaka wa fedha 2015/2016.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top