Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TRA YAITUNISHIA MISULI BANDARI YA DSM.



Mamlaka ya mapato Tanzania, TRA imetoa ufafanuzi juu ya Propoganda juu ya kupungua kwa mizigo/meli ktk bandari ya Dar kama ifuatavyo:-
1. Ni ukweli uliowazi kuwa kwa kiasi fulani mizigo imepungua kwa wastani wa asilimia 9-30 kutegemea na nchi,

2. Mizigo mingi iliyokuwa inapita bandari ya Dar kwa kisingizio inaenda Kongo siyo kweli ilikuwa inaenda Kongo badala yake ilikuwa wana-dump humu nchini,

2. Kudorora kwa bei ya shaba Zambia,

3. Uchaguzi Malawi
4. Stability Msumbuji kiasi kwamba bandari ya Beira imeanza kufanyakazi vizuri.

5. Kuanza kutumika kwa utaratibu wa Single Custom Territory ambapo mizigo inalipiwa ktk bandari ya Dar kabla ya kusafirishwa kwenda Kongo ambapo inawanyima wafanyabiashara kule Kongo kukwepa kodi n.k

6. Hali ya uchumi Duniani kwa ujumla.
7. Utafiti tulioufanya hata Bandari ya Mombasa mizigo imepungua.

Wakati meli zikiwa zimepingua ktk bandari ya  Dar,  Mapato yatokanayo na Forodha mwaka 2015 yalikuwa wastani wa Shilingi Bilioni 200-300  kwa mwezi.

Lakini tangu Disemba 2015 - August 2016 wastani wa mapato ya Forodha kwa mwezi ni Kati ya shilingi bilioni 400-550.

Facts hizi zipo Mwananchi yeyote anaweza kuzipata kwenye tovuti yetu ya TRA Taarifa za Mapato kila mwezi.

Taarifa ya Mapato ya August tutaitoa jumatatu na kila mmoja wenu apitie kwenye tovuti yetu ajiridhishe na kuondoa hofu kutoka kwa wachache wasiolitakia mema Taifa letu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top