Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TUCTA waunga mkono fao la kujitoa

Umoja wa vyama vya wafanyakazi na asasi za kiraia hapa nchini umeitaka serikali na bunge kutopitisha muswada unaondoa fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwani kufanya hivyo ni kuwakandamiza wafanyakazi.

Muswada huo ambao utaruhusu bunge linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma kufanya mabadiliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii na kuondoa fao la kujitoa  ambalo linamruhusu mfanyakazi kuchukua mafao yake mara tu anapoacha kazi hata kama hajafikisha umri wa kustaafu ambao ni miaka 60 au kustaafu kwa hiari suala ambalo vyama vya wafanyakazi zikiwemo asasi za kiraia vinalipinga kwa madai kuwa kuondolewa kwa fao hilo ni kuwakandamiza wafanyakazi na kuwanyima fursa ya kutumia fedha walizochuma kwa jasho lao.

Wafanyakazi wanalitaja  fao la kujitoa ambalo linamruhusu mwanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kudai fedha zake muda wowote anapoondoka  kazini kwa ajili ya kujikimu na hivyo kuondolewa kwake kutaondoa dhana ya mifuko hii ya hifadhi ya jamii ambayo ilianzishwa kwa lengo la  kumsaidia mwanachi kuendeleza maisha yake hata kama hayuko kazini.

Miongoni mwa malalamiko  ambayo wafanyakazi wanayo juu ya muswada huu ni serikali kutowashirikisha wadau katika kuuandaa na hivyo kutaka serikali kuurudisha kwao kuufanyia marekebisho kabla ya kwenda kujadiliwa bungeni.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top