Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ubungo, Kinondoni wagawana rasmi Madiwani

Meya wa Mnaispaa ya Kinondoni Boniface Jakob

Dar es Salaam. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jioni hii imewagawanya rasmi madiwani wake kwenda Manispaa mpya ya Ubungo na wengine kubakia Kinondoni kulingana na jiografia ilivyo.

Uamuzi  huo unatokana na Serikali kutangaza wilaya mpya za Ubungo na Kigamboni hatua itakayoifanya Dar es Salam kuwa na wilaya tano kutoka tatu za awali.

Meya wa Kinondoni, Boniface Jacob amesema uamuzi  huo umefikiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani usiku huu.

Amesema kabla ya uamuzi huo, vikao mbalimbali vya kiutendaji vilifanyika ambavyo pia vilizungumzia  mgawanyo wa rasirimali pamoja na watumishi.

"Baada ya siku 14 tunatarajia wakurugenzi wa Manispaa za Kinondoni na Ubungo wataitisha uchaguzi wa kumpata Meya na Naibu meya," alisema Jacob.

Kwa mujibu wa Jacob, Kinondoni itabaki na kata 20 wakati Ubungo itakuwa na kata 14.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top