Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Ikungi waanzisha mfuko wa Elimu

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu  akitoa maelekezo wakati alipokutana na kamati ya mfuko wa elimu ya wilaya.

 Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi Haika Massawe akichangia hoja wakati wa kikao cha wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya.
Mjumbe mwakilishi wa madhehebu ya dini sheikh Salum Ngaa akichangia hoja wakati wa kikao kilichoongozwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu pichani wakiwa  na wajumbe wa kamati ya mfuko  wa elimu wilaya.
Mkuu wa Wilaya Ikungi Miraji Mtaturu katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya mfuko wa elimu wilaya na viongozi wa halmashauri  baada ya kumaliza kikao nao.
                           ...................................................................................................................................................
MKUU wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu amekutana na kamati ya mfuko wa elimu wilaya na kuwaomba kuwa wazalendo katika kutafuta njia za kutatua changamoto za elimu wilayani humo.
Mfuko huo umeundwa baada ya uanzishwaji wake kuridhiwa na kikao cha baraza la madiwani kilichoketi hivi karibuni.
Akizungumza katika kikao cha kuwapatia majukumu yao  Mtaturu amesema  mfuko huo utakuwa na jukumu la kuratibu masuala yote yatakayosaidia kuboresha utoaji wa elimu katika shule za msingi na sekondari.
“nawapongezeni kwa heshima mliyopewa ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa kamati hii,naimani kuwa mtafanya kazi kwa uzalendo mkubwa ili matunda ya uwepo wenu yaonekane kwa kuitoa elimu yetu hapa ilipo na kuipeleka mbali zaidi,”alisema Mtaturu.
Alisema wakifanikiwa kuondoa changamoto zilizopo watakuwa wameboresha mazingira ya utoaji elimu na kuongeza ufaulu wa watoto jambo ambalo waliazimia walipokutana wadau wa elimu.
Akitoa taarifa kwenye kikao hicho katibu wa mfuko huo Salum Athuman alisema ili kutatua changamoto za elimu zilizopo katika wilaya hiyo zinahitajika jumla ya shilingi bilioni 26 kwa ajili ya miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa,nyumba za walimu,maabara,matundu ya vyoo na mabweni.

Aidha mwenyekiti wa kamati hiyo Hamis Maulid  kwa niaba ya wajumbe alisema wamepokea kazi hiyo na wataifanya kwa uadilifu mkubwa ili malengo yaliyokusudiwa yatimie.

Disemba  mwaka jana mkuu wa wilaya huyo alikutana na wadau wa elimu  ili kubaini changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ambapo waliweka maazimio yapatayo 37 yenyek ulenga kuboresha elimu wilayani humo na moja ya mkakati waliouweka ndio umezaa wazo la kuanzishwa kwa  mfuko huo wenye wajumbe 15 ambao  wameanza kazi rasmi ili kutafuta njia ya kutatua changamoto za elimu wilayani humo.


Wilaya hiyo ina jumla ya shule za sekondari 30 ikiwemo za kidato cha sita 3 na shule za msingi 108.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top