Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Lema ammwagia sifa Mbunge wa CCM

Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Goodbless Lema amemshukuru Mbunge Lazaro Nyalandu kwa kufanikisha safari ya Marekani ya watoto watatu ambao walinusurika kifo katika ajali ya basi la shule ya Lucky Vicent iliyotokea Karatu na kusababisha vifo vya watu 35.

Mh. Nyalandu alikuwa bega kwa bega na kufuatilia kila hatua kuhakikisha watoto hao pamoja na wazazi wao na daktari wanasafiri kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kupata matibabu zaidi. 
"Mh Lazaro Nyalando , Mungu akubariki sana kwa kazi nzuri ya kusaidia watoto waliopatwa na ajali hapa Arusha, jitihada zako Mungu atakulipa" alisema Godbless Lema 

Katika hatua nyingine Mh Lazalo Nyalandu ameomba pesa zitakazo endelea kuchangwa na Watanzania na watu wengine duniani kwa ajili ya watoto hao zitumike kujenga ICU katika hospitali ya Mount Meru. 

"Kwa kuwa wadau wanaendelea kuchangia na kwa kuwa shule ya sekondari zimekubali kuanzisha mfuko ambao wanausimamia wenyewe na kwa kuwa mfuko huo lengo lao kubwa lilikuwa kuwasafirisha hawa watoto kazi ambayo imefanywa na Samaritan Purse lakini lengo la pili ilikuwa ni kwenda kuwatibu kazi ambayo inafanywa na Shirika la STEMM kwa kushirikiana na Hospitali kuu ya Mercy hivyo kazi itakayobaki Mh Mkuu wa Mkoa itakuwa ndogo, kwa hiyo nimeomba na nimeshaurina nao na wamekubali kwamba Watanzania na wanadunia wote watakao endelea kuchanga fedha zote ziletwe kwako Mh Mkuu wa mkoa ili ziweze kujenga kituo cha wagonjwa ambao wanahitaji huduma ya haraka (ICU) katika hospitali yetu ya Mount Meru" alisema Nyalandu 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top