Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mti wa maajabu .... Wapaza sauti, watokwa na machozi ya damu wakati ukikatwa


Wakazi wa Barabara ya Iloganzala  Jijini Mwanza jana walipigwa butwaa baada ya mti kutoa sauti kama binadamu ukipinga using'olewe. 

Tukio hilo limetafsiriwa kuwa la kishirikina ama mazingaombwe ikizingatiwa kwamba si jambo lenye uhalisia mti kuongea kama binadamu. 

Katika eneo la Iloganzala Jijini Mwanza kuna upanuzi wa barabara inayoelekea Uwanja wa ndege wa Mwanza. 

Shughuli ya kuung'oa mti huo aina ya mwembe  leo imeendelea ikiwa ni siku ya pili ya kukabiliana na mwembe huo na hatimaye wamefanikiwa kuung'oa huku mamia ya wananchi wakishuhudia tukio hilo la ajabu

==>Tazama Video hapo chini

MAAJABU YA MWEMBE MWANZA!!

Leo jijini Mwanza maeneo ya Shule ya Msingi Isenga mamia ya watu Wamekusanyika kushuhudia Mti wa ajabu ulioongea!

Tingatinga la Ujenzi wa barabara ya Airport liliufikia Mti huo ili kuukata na ndipo ukasema "Msinikate Jamani Naumia" na ndipo dereva wa Tinga tinga alipoishia kupiga Mayowe na watu kujaa, ...ingawa Baadae tinga tinga lilifanikiwa kuukata na Mizizi yake kuanza kutoa Damu kwa mujibu wa Mashuhuda.

Kuhusu huu Mti ndugu zetu wenyeji wana Mengi ya kutueleza  maana Muda huu kama unavyoona hapo pichani Mti umeshaondolewa na Wananchi wapo bize wanaushambulia kwa kugawana vipande kwamba vinawafaa katika Biashara zao na wengine wanaenda kutengeneza dawa!
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top