Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwenyekiti kijiji cha Ikungi atumbuliwa

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizungumza na wananchi hawapo pichani kwenye mkutano maalum wa kijiji cha ikungi,kulia kwake ni kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho Athuman Seleman na kushoto kwake ni  kaimu mkurugenzi wa halmashauri  Haika Massawe.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu katikati akiwa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Haika Massawe na kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho Athuman Seleman wakiwa kwenye mkutano maalum wa kijiji.

Mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya Ikungi Kitundu Mkumbo akisoma taarifa ya ukaguzi mbele ya mkutano maalum wa kijiji cha Ikungi.


 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ikungi  waliohudhuria mkutano maalum wa kijijji hicho wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu hayupo pichani.


Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ikungi  waliohudhuria mkutano maalum wa kijijji hicho wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu hayupo pichani.
............................................................................
MKUTANO maalum wa Kijiji cha Ikungi wilayani Ikungi mkoani Singida umemuondoa Mwenyekiti wa kijiji hicho Hussein  Ikusi kutokana na matumizi  mabaya ya madaraka kwa kufanya ubadhirifu wa mali za kijiji zenye thamani ya shilingi milioni 9.

Ubadhirifu huo aliufanya  toka alipoingia madarakani mwaka  2014 akishirikiana na aliyekuwa mtendaji wa kijiji hicho Hamis  Isango aliyehamishiwa kijiji cha Irisya.

Hayo yalibainika baada ya halmashauri ya kijiji kuitisha kikao maalum tarehe 24 aprili mwaka 2017 wakimtuhumu mwenyekiti kwa hoja zipatazo 5.

Hoja hizo ni kushindwa kusimamia mali za kijiji,kushindwa kusimamia mipaka ya kijiji,kushindwa kuonyesha ushirikiano na uongozi wa halmashauri ya wilaya,Ofisi ya mkuu wa wilaya na taasisi za serikali zilizopo wilayani,kuwa chanzo cha migogoro badala ya kuwa mtatuzi na kushindwa kusimamia usomaji wa mapato na matumizi ya kijiji kwa mujibu wa sheria kwa kipindi cha  miaka miwili na nusu.

Ubadhirifu huo umebainishwa na mkaguzi wa mahesabu ya ndani Kitundu Mkumbo aliyeagizwa na mkuu wa wilaya hiyo Miraji Mtaturu kufanya ukaguzi wa mapato na matumizi ya kijiji baada ya kupokea tuhuma kuhusiana na mwenyekiti huyo.

Akizungumza katika kikao cha kutoa taarifa kuhusiana na maamuzi yaliyoafikiwa na halmashauri ya kijiji Mtaturu alimuagiza kaimu  mkurugenzi wa halmashauri Haika Massawe kumsimamisha kazi  mtendaji wa kijiji cha Irisya Hamis Isango aliyehamishiwa kijiji kingine ili arudi ikungi kujibu tuhuma za kuondoka na vitabu 12 vya kukusanyia mapato alivyoshindwa kukabidhi wakati anahama ikiwemo na  kutoa maelezo ya fedha zilizoonekana kupotea mikononi mwake.

"Bwana Ikusi kabidhi fedha na mali kama ushauri wa mkaguzi wa mahesabu alioutoa hapa  mbele ya wananchi"alisisitiza Mtaturu.


Aprili 24 mwaka huu halmashauri ya kijiji  iliazimia kwa kauli moja kumuondoa mwenyekiti huyo kutokana na tuhuma hizo dhidi yake huku huku ikisisitiza  kuwa Usimamizi wa Rasilimali za Umma ni mabadiliko Chanya kwa maendeleo ya Ikungi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top