Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC Makonda atoa maagizo 17 kwa watu wa Sekta ya Ardhi na Ujenzi




RC MAKONDA ATOA MAELEKEZO 17 KWA WATENDAJI WA SEKTA YA ARDHI NA UJENZI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 akizungumza Na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ametoa maelekezo 17 ya kuzingatia katika utendaji wao.

1.Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi  Kushughulikia migogoro ya ardhi Na Ujenzi ili wananchi wasipeleke malalamiko yao ngazi za juu.

2.Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi Wameagizwa kutoa vibali vya Ujenzi ndani ya mwezi mmoja Na zoezi hilo lianze Mwezi wa sita mwaka huu 2017. Mwanzoni mwa mwezi wa Saba kuzinduliwa teknolojia ambayo wananchi watapata taarifa zao za Ardhi kwenye mtandao Jambo ambalo litafanya Dar es salaam kuwa kiganjani mwa wananchi.

3.Wakuu wa Idara katika Sekta ya Ardhi Na Ujenzi  kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu Mipango ya Idara kwenye vyombo vya habari kwa kuwatumia maafisa habari kwani tayari wana mahusiano Na waandishi mbalimbali katika vyombo vyombo vya habari.

4.Wakuu wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kutoa TAARIFA ya maeneo yote ya wazi yaliyotolewa Hati, Na kujitokeza haraka kwa wote waliotoa Hati za maeneo ya wazi kama wapo.

5.Wakuu wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kusimamia haraka upimaji wa maeneo yote ya Umma kama kama vile Shule, Hospitali, Na Masoko kama alivyoagiza Waziri wa TAMISEMI sambamba Na kutoa Mikakati wa Upimaji.

6.Wakuu wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kuhakikisha ufanisi Na bidii ya utendaji inaongezeka hususani mikakati ya kuhusisha wapimaji binafsi wanaotambulika kwani Mji ukipimwa vyema Madiwani watafurahi lakini pia itakuwa njia rahisi ya kuepuka migogoro ya Ardhi.

7.Kushughulikia changamoto za kisera unaofanya utaratibu wa Upimaji Na utoaji wa Hati kuchelewa kukamilka.

8.Mabaraza ya Kata kuangaliwa upya kwa mujibu wa Sheria ili kuwa Na utendaji imara unaoshabihiana Na Jambo la kisera.

9.Kila Mtumishi kufanya Kazi yake kwa Uaminifu kwani dhamani aliyopewa ni kubwa Na anapaswa kuitendea Haki. Watumishi wote kusimamia Na kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani chama hicho ndicho kimeingia mkataba Na wananchi katika kipindi cha miaka mitano.

10.Kila Mkuu wa Idara kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015-2020 ili kutambua maelekezo yaliyobainishwa katika Sekta yake sambamba Na kuwaelekeza wasaidizi wao pia kuisoma Na kuielewa vyema ilani hiyo.

11.Kufatilia Na kufahamu upandaji wa madaraja Na stahiki zao kwani ni Haki zao za msingi kisheria ikiwa ni pamoja Na kwenda likizo.

12.Watumishi wote kuheshimu mamlaka walizonazo Na kutumia vikao halali kutoa taarifa sahihi kwa watu husika.

13. Kuwa Na ushirikiano wa watumishi katika Idara zote ili kukuza ufanisi wa Kazi.

14.Kujitokeza ndani ya wiki moja kwa watumishi wote wa Sekta ya Ardhi waliojihusisha Na utoaji wa Hati za Ardhi kinyume Na sheria. Na endapo wasipojitokeza Na wakabainika watachukuliwa hatua za kisheria.

15.Kufafanua baadhi ya mambo ili Madiwani waweze kuelewa. Sambamba Na kutoogopa maadhimio kama wanatenda Kazi kwa mujibu wa Sheria pasipo kupendelea.

16.Wakuu wa Idara kila mwisho wa wiki kutoa taarifa kwa Wakurugenzi inayoonyesha idadi ya Migogoro Na jinsi ilivyotatuliwa.

17.Katika kupunguza changamoto ya kuwafikia wananchi kwa Wakati RC Makonda Amesema atatoa Pikipiki 5 Katika Sekta ya Ardhi kwa kila Manispaa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top