Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Said Meck Sadik aeleza sababu za kung'atuka


Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, amesema ameamua kuondoka Serikali baada ya utumishi wa muda mrefu na anakwenda kupumzika mkoani Mwanza huku akiwa mfugaji wa samaki. 

Aidha Sadiki alisema pia kulingana na afya yake, anahitaji kupisha vijana wadogo wamsaidie Rais Dkt John Magufuli kulingana na kasi yake kwani yeye ameepuka kumkwaza Rais wakati wa utekelezaji wa majukumu yake kama mkuu wa mkoa. 

Uamuzi huu wa kupumzika nilimuomba rais muda mrefu sana, na nikirudi Kijijini nitaendelea na ufugaji wa samaki maana nilishaandaa bwawa la kufugia, nitaendelea nalo huku nikiwaza jambo lingine la kufanya," alisema. 

Sadiki alisema hayo jana wakati wa mahojiano maalumu na Habari leo kuhusu sababu zilizochangia kumuomba Rais Magufuli kuacha kazi yake ya ukuu wa mkoa wa Kilimanjaro. 

"Namshukuru Rais kuridhia ombi langu, nimetumikia Serikali tangu mwaka 1999 nikiwa mkuu wa wilaya na baadaye mkuu wa mkoa kuanzia mwaka 2005 hadi sasa ninapoondoka mwenyewe..nimeona ni wakati muafaka kumweleza aliyeniteua kuwa nahitaji kupumzika nikiwa na akili timamu na afya njema", alisema. 

"Kama kiongozi muungwana lazima ifike mahali ukiri kwamba wapo vijana wenye uwezo mzuri na kasi ambayo inaendana na serikali ya awamu ya tano.. mimi nilishatekeleza wajibu wangu na mchango kwa serikali yangu, sasa inatosha, tupate mawazo na michango ya wengine", alisema. 


Sadiki ambaye amekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro tangu Machi 13,2016 alipoteuliwa na Rais Magufuli, alisema siyo vibaya kwa kiongozi kujitathimini na kuwaachia wengine kama atabaini kasi yake ya utendaji kazi imeanza kupungua.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top