Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri wa Elimu atumbua vigogo TIE

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako leo Jumatatu jioni amewasimamisha kazi Kaimu Kamishna wa Elimu, Nicholas Bureta na Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Tanzania (TIE), Dr. Elia Kidga kufuatia sakata la kasoro zilizopo katika vitabu vya kujifunzia wanafunzi.

Waziri Ndalichako ametangaza hatua hiyo kufuatia kuibuka kwa mjadala bungeni leo jioni kuhusu kasoro kwenye vitabu hivyo ambavyo vimechapishwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kufundishia. Miongoni mwa makosa yaliyobainika kwenye vitabu hivyo, ni kurasa ulioandikwa kuwa Dodoma ndio mji mkubwa Tanzania.

Waziri Ndalichako amewasimamisha viongozi hao na ameliambia bunge kuwa uchunguzi wa kina unafanyika na baada ya kukamilika hatua za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika.

Wabunge walitishia kuzuia kupitisha bajeti ya Wizara ya Elimu hadi hapo wizara itakapotoa uamuzi wenye mantiki katika kutatua tatizo hilo lililozua mvutano mkubwa.

“Kwa mamlaka niliyonayo, namuagiza Kaimu Kamishna wa Elimu na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), kuondoka ofisini mara moja ili kupisha uchunguzi,” alisema Ndalichako

Baada ya waziri kutoa agizo hilo, wabunge waliridhia kupitisha bajeti ya wizara hiyo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top