Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HAMA HAMA YA CHADEMA KUJIUNGA CCMNashtushwa na wimbi kubwa la vigogo wa Chadema kukacha chama chao na kujiunga na CCM. Vigogo hao ni Wenyeviti wa Chama, Madiwani, wenyeviti wa Serikali za mitaa, kijiji na kitongoji, makada na wanachama maarufu wa Chadema.

Nimetafakari kwa kina hii hama hama nikaishia kukumbuka misemo ya Wahenga mikuu miwili ambayo ni "Jasiri haachi asili" pamoja na "Usimlazimishe Tembo kunyw maji".

Nikaendelea kukumbuka namna ambavyo Chadema ilivyompata mgombea Urais kwa hati ya dharura maana hakutarajiwa kupokelewa wala kukubaliwa kuwa mgombea lakini ajabu akafanikiwa. Nikaendelea kukumbuka namna ulivyoundwa umoja wa haraka haraka wa vyama vya Upinzani na namna wagombea wa nafasi mbalimbali walivyopatikana.

Ile misemo niliyoikumbuka na mazingira yote ya uchaguzi yalivyokuwa ndiyo ambayo inaitafuna Chadema kwa sasa.

Wale Madiwani, Wenyeviti wa mitaa na vitongoji wanaosemekana kununuliwa kipindi cha nyuma kutoka CCM wakadhani labda wanaikomoa CCM sasa wameamua kurudi nyumbani kwao kwenye asili yao.

Pesa zina mipaka yake isiyoweza kumlazimisha mtu kuamini, kufikiri wala kupinga mambo milele.  Unawezaje kumlazimisha mtu ANAEJITAMBUA kupinga kila kitu?

Wapo wanayoyaona mazuri na ya muhimu kwao yanayofanywa na Serikali madhubuti ya CCM inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli ambayo ni MWENDAWAZIMU pekee anaweza kupinga ila wanashangaa hata wao wanaojitambua kulazimishwa kupinga tu, wamegoma katika hili ndio maana wenyewe wameamua kwa hiari yao kurudi CCM.

Binafsi siombei sana chama hiki kife lakini naona bora kife tu kwani hakikidhi kigezo hata kimoja kuitwa chama kikuu cha upinzani popote pale ulimwenguni.

Tunaomba maamuzi yao ya kujiunga na CCM yaheshimiwe kama CCM walivyoheshimu maamuzi ya Kingunge, Sumaye, Lowassa nk!! Hiyo ndio SIASA SAFI!!

Shilatu E.J
Nashtushwa na wimbi kubwa la vigogo wa Chadema kukacha chama chao na kujiunga na CCM. Vigogo hao ni Wenyeviti wa Chama, Madiwani, wenyeviti wa Serikali za mitaa, kijiji na kitongoji, makada na wanachama maarufu wa Chadema.

Nimetafakari kwa kina hii hama hama nikaishia kukumbuka misemo ya Wahenga mikuu miwili ambayo ni "Jasiri haachi asili" pamoja na "Usimlazimishe Tembo kunyw maji".

Nikaendelea kukumbuka namna ambavyo Chadema ilivyompata mgombea Urais kwa hati ya dharura maana hakutarajiwa kupokelewa wala kukubaliwa kuwa mgombea lakini ajabu akafanikiwa. Nikaendelea kukumbuka namna ulivyoundwa umoja wa haraka haraka wa vyama vya Upinzani na namna wagombea wa nafasi mbalimbali walivyopatikana.

Ile misemo niliyoikumbuka na mazingira yote ya uchaguzi yalivyokuwa ndiyo ambayo inaitafuna Chadema kwa sasa.

Wale Madiwani, Wenyeviti wa mitaa na vitongoji wanaosemekana kununuliwa kipindi cha nyuma kutoka CCM wakadhani labda wanaikomoa CCM sasa wameamua kurudi nyumbani kwao kwenye asili yao.

Pesa zina mipaka yake isiyoweza kumlazimisha mtu kuamini, kufikiri wala kupinga mambo milele.  Unawezaje kumlazimisha mtu ANAEJITAMBUA kupinga kila kitu?

Wapo wanayoyaona mazuri na ya muhimu kwao yanayofanywa na Serikali madhubuti ya CCM inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli ambayo ni MWENDAWAZIMU pekee anaweza kupinga ila wanashangaa hata wao wanaojitambua kulazimishwa kupinga tu, wamegoma katika hili ndio maana wenyewe wameamua kwa hiari yao kurudi CCM.

Binafsi siombei sana chama hiki kife lakini naona bora kife tu kwani hakikidhi kigezo hata kimoja kuitwa chama kikuu cha upinzani popote pale ulimwenguni.

Tunaomba maamuzi yao ya kujiunga na CCM yaheshimiwe kama CCM walivyoheshimu maamuzi ya Kingunge, Sumaye, Lowassa nk!! Hiyo ndio SIASA SAFI!!

Shilatu E.J
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top