Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Madudu yafumuliwa soko kuu Singida Mjini .... Maagizo mazito yatolewaCHIEF YARED ABAINI MADUDU SOKO KUU SINGIDA MJINI

Katibu CCM Wilaya Singida Mjini Chief Sylvester Yaredi  11-7-2017 alitembelea soko kuu la Singida mjini kujionea shughuli za Soko baada yakuwepo kero kadhaa kutoka kwa wananchi.
mambo kadhaa yamebainika.
--Chemba za maji machafu zinaziba na hivyo kupelekea maji machafu kutiririka sababu ya kuziba ni mifuko ya Plastik
--Karavati za kufunika mitaro hakuna hivyo kusababisha hatari kwa wananchi.
-- Uwepo wa meza nje ya soko hivyo kuwakosesha wateja walioko sokoni ndani.
- -Soko kutofanyiwa usafi
-- paa la soko kwa baadhi ya sehemu kuchakaa na kupelekea maji kuvuja
- -baadhi ya kuta kuchakaa na kuwa hatarishi
- -kukosekana mageti ya milango ya kuingilia sokoni hivyo soko kuwa si salama
--Wafanyabiashara kupanga bidhaa njiani na kuziba njia za wateja wa soko.

Baada ya kujiridhisha upande wa Manispaa uKiwakilishwa na Afisa Usafi na mazingira Manispaa,Mhandisi usanifu majengo manispaa na Afisa biashara Manispaa Mwisho Katibu CCM wilaya alitoa maelekezo kwa Wahusika Kuhakikisha Changamoto zote zilizoibuka kuhakikisha zinafanyiwa kazi ndani ya Mwezi mmoja na nusu  ikiwemo usafi kuanza Jtano Tarehe 12 kusafisha soko zima na Katibu  kujionea hali ya usafi Ijumaa
pia Chemba zizibuliwe  

*"Afisa Mazingira ndani ya wiki moja hakikisha soko linakuwa safi buibui hazipo na chemba hazijaziba tena ili soko hili lifanane na hadhi ya Manispaa kwa sasa ni Aibu,Mpo mnafanya kazi gani kama hapa hamfiki? "*

pia ameutaka uongozi wa Soko kuhakikisha unawapatia meza ndani ya Soko kinamama wanaopanga kuuza vitu vyao nje ya soko chini, Na Soko kufanya uchaguzi wa Viongozi wake, Karavati pia kujengwa na kuwekwa ili kuepusha ajali,

Katika ziara hiyo Katibu Wilaya aliambatana na katibu Uvccm wilaya , Mhe Diwani kata ya Ipembe na Katibu Ccm kata ya Ipembe.Katibu CCM wilaya amempongeza Diwani wa kata ya Ipembe kwa ufuatiliaji na uchapakazi wake katika kuwahudumia wananchi.

Baadae mchana Katibu ccm wilaya Singida mjini alitembelea kujionea ujenzi wa High school pekee ya wananchi Singida mjini Iliyopo kata Mungu Maji na kuridhishwa na maendeleo ya Ujenzi ikiwemo Mchango mkubwa  wa mhe Mbunge Singida mjini katika ujenzi huo.
*CCM MPYA TANZANIA MPYA.*
*ILANI LAZIMA ISIMAMIWE KIKAMILIFU*
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top