Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Malinzi, Mwesigwa mambo bado magumu

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa wamerudishwa rumande kwa mara nyingine kutokana na upelelezi  wa kesi yao kutokamilika hivyo wamerudishwa tena Mahakamani Julai 31 mwaka huu shtaka lao litakaposomwa tena.

Uamuzi huo umetolewa katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, ambapo ndipo mashtaka hayo yalifunguliwa mara ya kwanza na kuendelea mpaka sasa.

Malinzi na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa na matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 yakiwemo kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top