Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Msukuma amwangukia Rais Magufuli

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM) amemtaka Rais Magufuli kutosikiliza kelele za baadhi ya viongozi hususani wapinzani na kusema anapaswa kushikilia hapo hapo aliposhikilia kwani anafanya vizuri na mambo anayotenda yameanza kuonekana.

Msukuma alisema hayo juzi wakati wa makabidhiano ya nyumba 50 zilizojengwa na taasisi ya The Benjamin William Mkapa Foundation (BMF) na kusema wao Geita wapo mstari wambele kuhakikisha wanaunga mkono kila jambo ambalo linafanywa na Rais Magufuli.

"Mhe. Rais sisi huku Geita tunakuunga mkono na tupo tayari kujitolea hata bure katika mambo unayofanya katika nchi hii, nakuomba tu usisikilize zile kelele za watubali wewe fanya kazi kwa ajili ya Watanzania, maana kuna watu wengine wanasimama bungeni na kuanza kupiga kelele tu, wengine wanasimama bungeni na kusema eti unajenga uwanja wa ndege Chato, usiwasikilize na wala kelele zao zisikukatishe tamaa, ukiona kitu kingine kizuri chochote usiusahau mkoa wa Geita" alisisitiza Msukuma

Mbali na hilo Msukuma alikuwa na ombi kwa Rais Magufuli pindi wawekezaji waliokuwa wakisafirisha makinikia kwenda nje ya nchi wakilipa deni hilo basi awakumbuke watuwa Geita japo kwa barabara za lami kwani barabara anadai zimekuwa hazina kiwango kizuri na ni mbovu.

"Sahizi ukizinguka sehemu ukisema tumetoka Geita kidogo tunakuwa na heshima kwa ajili yako Rais Magufuli, tunakuomba uendelee hivyo hivyo ombi letu watu wa Geita, mgodi huu hatufadiki nao, kwa kuwa tulipitisha asilimia 6 tunaomba asilimia 1 tubaki nayo, lakini ombi letu la pili tumekusikia mara nyingi unasema wawekezaji wakubwa wamekuwa na maeneo makubwa maeka na maeka, tunaomba vijana wako waruhusu wawekezaji wapunguze maeneo ili vijana wachimbaji wadogo wakachimbe madini," alimalizia Msukuma

Mbali na hilo Rais Magufuli alimsifu sana mbunge msukuma na kusema hata bungeni huwa anamsikia anasimamia sana chama chake (CCM) na kusema kuwa yupo vizuri sana kwa jambo hilo, kwani anawakilisha vizuri sana.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top