Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Polepole: Wapinzani hawana nidhamu

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kwamba wapinzani wameonyesha utovu wa nidhamu hivyo amewahakikishia kuwa atawapokea wanachama wanaohama kuanzia sasa kwani anaorodha ndefu ya watu wanaotaka kuhama kutoka upinzani na kuja CCM.
Polepole amesema amemua kuchukua uamuzi huo baada ya CHADEMA kuonesha utovu wa nidhamu kwa kudai kuwa madiwani wanaokihama chama hicho wamehongwa na CCM.
“Wapinzani hawana nidhamu Sasa tutaanza kumchomoa mmoja baada ya mwingine na kwa kutekeleza hilo wiki hii tutampokea kiongozi wao mkubwa,’’amesema Humphrey Polepole akiwa mjini Bagamoyo.
Akitaja watu hao Polepole amesema kuwa anaorodha ya Wenyeviti, Madiwani na Wabunge lakini siku nyingi tu alikuwa amewakatalia kuwapokea.
“Madiwani wamesema wanamuunga mkono Rais Magufuli, wametoka wenyewe wameanza kusema CCM imewanunua, sasa kwa vile wameanza utovu wa nidhamu nitaanza kumtoa mmoja baada ya mwingine,’’amesema Polepole huku akisisitiza kuwa alikuwa anawakataa watu wanaohamia CCM kutoka upinzani.
“Nilikua nakataa kuwapokea ila nina orodha kubwa wapo wenyeviti, wabunge kibao kama vile watu wanaojisaliji kodi ya majengo TRA…Unajua wanaosema wanaisoma namba, nawahakikishia baada ya miaka mitano kwa spidi hii iliyoanza nayo CCM namba inayoonekana wakati huu itakuwa haisomeki kabisa, nitafanya shoo ndogo tu kuwachomoa viongozi hao sipendi kwenda kuwachukua wengi sababu nitaonekana kama nawahujumu vile na pia ili upinzani usikose watu angalau wa kuzungumza nao,“.amesema Humphrey Polepole.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top