Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Shaka afanya maajabu Kigoma












*YALIYOJIRI LEO JUMATATU 17/07/2017 KATIKA ZIARA YA KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC) MKOA WA KIGOMA WILAYA YA UVINZA*

- Amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa mashina na matawi wapya waliochaguliwa wa chama na jumuiya zake kutoka katika kata zote za wilaya Uvinza.

-Ametembelea na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM,  Jengo  jipya la wakinamama na sehemu ya jengo  la upasuaji katika kituo cha afya Nguruka  ambapo pia alikabidhi  msaada wa vifaa tiba mbali mbali  pamoja na kutoa sabuni kwa wagonjwa waliolazwa wodi ya watoto na akinamama wajawazito.

-Wakati huo huo vijana wa CCM waliendesha harambee ya kuchangia mashuka 40, shuka 20 zimechangiwa na mbunge wa viti maalum Mhe Zainab Katimba alichangia shuka  20,  katibu  hamasa UVCCM wilaya ya Uvinza alishangia shuka 20, viti  20 na meza 3 zilichangiwa na mwenyekiti wa kijiji cha Nguruka kwa ajili  kituo hiko  cha afya.

-Amekabidhi msaada ya machine mbili za kufyatulia matufali kwa vikundi vya vijana toka kata mbili za nguruka na nyangabo kisha kuzungumza na vijana hao.

-Ametembelea na kufanya mazungumzo na vijana  waliojikusanya kufanya shuhuli za ujasiriamali  ikiwa ni sehemu ya kuitikia wito wa Mhe Rais  Magufuli kwa vijana kujituma na kufanya kazi ili kuinua kipato chao.

-Amekabidhi kadi mpya za CCM na kupokea wanachama wapya waliohama 82  toka vyama vya CUF, ACT wazalendo na NCCR Mageuzi katika kata ya Nguruka.

-Ametembelea mradi wa vijana wa kuuza mbegu na pembejeo za kilimo.

-Amezungumza na vijana, wanakimama na wazee wa CCM  katika kata ya Kazuramimba ambapo  jumla ya vijana 226 kutoka CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na ACT wazalendo wamerudisha  kadi na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

-Wakati huo amekabidhi kadi kwa wanachama wa CCM  na UVCCM  walitimiza masharti ya uanachama  kikatiba na kikanuni.

Jioni leo Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) amewasili wilaya ya Kigoma Mjini kuendelea na Ziara jumanne 18/07/2017  katika wilaya hiyo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top