Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UVCCM wamvaa Tundu Lissu

Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umesema matamshi ya kilofa na kipumbavu yaliotamkwa na Mbunge wa Singida Mashariki(Chadema) Tundu Lisu ni ya kusaka umaarufu wa kisiasa hatimae   awanie  urais akiwawacha solemba  Edward Lowassa na mshirika wake Fredrick Sumaye .
Aidha Umoja huo umesema povu linalowatoka viongozi wa upinzani akiwemo Lisu, ni kielelezo cha kutapatapa na kufilisika kisiasa kufuatia utendaji unaokubalika wa serikali   ya Rais John Magufuli huku  wakionekana kuvunjika matumaini na kukata tamaa. 
Hayo yametamkwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM  Shaka Hamdu Shaka wakati alipozumguza na viongozi, wanavyuo, makundi ya vijana, wanachama wa CCM na jumuiya zake  katika ukumbi wa CCM  Kizota mjini kigoma mkoani hapa. 
Shaka alisema maneno ya Lisu hayawezi kuitingisha serikali ya CCM  na kwamba serikali inayoinanga iwapo  itamtaka akamatwe kwa kuvunja sheria za nchi, vyombo vya  dola havitasita kumuweka kizuizini.
Alisema kuna kila ishara ya mwanasiasa huyo wa upinzani inayoonyesha akiyatamani maisha ya gerezani  baada ya kuchoshwa na yale ya uraiani ambapo sasa ameamua kutamka upuuzi, kujeli  kinyume na ustaarabu.
"Tumemtafakari na kubaini ana nia ya kuwania urais mwaka 2020, anachotaka ni kuwaacha kwenye mataa jamaa zake kina Lowasa na sumaye, ila ajue akizidi kueneza matamshi ya kipuuzi anaweza kukamatwa na kutupwa mahali"Alieleza shaka 
Alisema hakutawakuwa hakuna maana ikiwa mtu mmoja anainanga Serikali na kuipaka matope, kumkejeli Rais aliyewekwa kisheria na kikatiba na wananchi akaendelea kutazamwa macho. 
"Lisu si kama papai ambalo kama likiwekwa ndani litaooza na kuharibika, anaweza kukaa huko kwa usalama wake na wa nchi, tumeruhusiwa kisheria kufanya siasa za vyama vingi kwa ustaarabu na uungwana na si kufanyiana kejeli na dhihaka "Alieleza 
Alisema hata wakati wa utawala wa Baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere walikuwepo baadhi ya wanasiasa waliotaka kuidharau serikali, walikamatwa kwa usalama wao na kuhifadhiwa mahali kwa muda fulani kwa maslahi ya nchi. 
"Lisu ni nani mbele ya mamlaka za kisheria na kikatiba, tunadhani anataka nyingi nasaba hivyo ajiandae siku yoyote anaweza kukutwa na msiba, msiba wa kujitakia hauna pole, dola yoyote haifanani na kitambaa cha deki" Alisisitiza. 
Uvccm ina ushahidi wa kutosha toka kwa watu wa karibu na Lisu wamemwambia kwamba ndiye anayetosha kuwania urais ndani ya chadema mwaka 2020 hivyo ametakiwa atafute "kick' ya kisiasa ili kumvuruga Sumaye na Lowassa .
Hata hivyo shaka alisema si kosa kwa Lisu kuwania urais ila anachotakiwa ni kujipima kibusara,  kiuwezo na kiupepo kama ni mtu anayestahili na sahihi ambaye  anayetosha kuomba nafasi hiyo au la.
Vile vile uvccm umewataka watanzania kumpuuza mwanasiasa huyo wa chadema kwa kadri atakavyotamka kwasababu mtu yoyote mwenye ufahamu na uelewa hawezi kudhihaki mamlaka ya Rais na nafasi alionayo. 
"Ujasiri wa kuidhihaki mamlaka ya Rais ni sawa na mtu juha au punguani anayejaribu kutupa jiwe katikati ya mzinga wa nyuki au mpumbavu kumchezea simba sharubu "Alieleza shaka. 
Kaimu huyo katibu mkuu Shaka  aliwashukuru wazee wa mkoa wa kigoma kwa kumtawaza na kuwa mwana kigoma huku akiwahidi hatawangusha ila malipo anayoyaanda kuonyesha shukran na furaha yake ni kuongoza harakati za kisiasa zitakazomuondoa Zito Kabwe kwenye nafasi ya ubunge wa kigoma mjini mwaka 2020 . 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top