Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Bangi zamponza Mbunge wa Chadema John Heche

Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche jana alikamatwa na polisi  alipokwenda kituo cha polisi cha Tarime  kufuatilia kukamatwa kwa Katibu wake.

Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba amesema kuwa polisi walimkamata Heche kutokana na kauli zake ikiwepo kauli ya kutaka kilimo cha bangi kihalalishwe pamoja na kauli yake ya kuzuia shughuli za ACACIA.

"Mhe. Heche alifika Polisi Tarime kwa ajili ya kufuatilia kukamatwa kwa Katibu wake, katika hali ya kushangaza naye akawekwa chini ya ulinzi na RCO na baadae kuelezwa kuwa alikuwa akitafutwa kwa makosa mawili 

"Kosa la kwanza ni  Kauli aliyoitoa mapema mwaka huu katika mkutano wa hadhara Sirari ya kwamba atapeleka hoja bungeni aiombe serikali ihalalishe kilimo cha bangi na pili kauli yake ya hivi karibuni kuhusu kuzuia shughuli za ACACIA Nyamongo kufuatia Kauli ya Rais kwamba mgodi huo haupo kihalali nchini." alisema Marwa Ryoba

Aidha Mbunge Marwa anasema kuwa Heche alikataa kutoa maelezo yoyote polisi na jeshi la polisi limechukua simu zake zote

"Walimwachia Heche ila wakachukua simu zake zote na kumtaka afike polisi Jumatatu kwa mahojiano. Alikataa kuchukuliwa maelezo yoyote kwa kuwa hakuwa amekwenda Polisi kwa mambo hayo bali kushughulikia kukamatwa kwa Katibu wake, hivyo amejidhamini na kuondoka ila simu zimebaki Polisi" alisema Marwa Ryoba
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top