Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Bomba la Mafuta fursa kwa Watanzania



Naungana na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Magufuli na Serikali yake pamoja na Rais Mseveni wa Uganda kwa kuandika historia mpya ya ushirikiano wenye tija.

Historia inaandikwa kwa nchi mbili za Tanzania na Uganda ambapo jiwe la msingi linawekwa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani bandari ya Tanga nchini Tanzania ambapo jiwe la msingi la kuanza ujenzi huo litawekwa.

Ni heshima Kubwa nchi yetu ya Tanzania kupata fursa hii ya bomba la mafuta kupita nchini Tanzania.

Kuna faida nyingi sana kama Taifa tutapata kutokana na uwepo wa mradi huu wa bomba la mafuta.

Wakati wa ujenzi Watanzania wengi watapata fursa ya ajira ambapo jumla ya ajira 40,000 zitapatika. Ajira za ufundi, ulinzi, upishi, usafiri, fursa za malazi, na huduma za kifedha.

Ukiachilia mbali fursa hiyo mradi huu utapelekea kufunguka kwa Ukanda wa Biashara kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki kama vile Rwanda, Burundi, Kongo, Sudan ambapo wanaweza kuunganishwa na miundombinu hiyo na kusafirisha mafuta kwa urahisi.

Kukamilika kwa mradi huo nchi za Tanzania na Uganda zitapata mapato na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wake.

Faida nyingine ya bomba la mafuta kuwa ni pamoja na gharama za mafuta kupungua kutokana na nchi za Afrika Mashariki kutumia mafuta yake yenyewe kwenye magari pamoja na ndege hivyo kuchochea kasi ya utalii katika nchi husika pamoja na ajira.

Gharama ya mafuta itakapo pungua ni dhahiri gharama za usafiri, usafirishaji na bidhaa nazo pia zitapungua. Maisha kuwa rahisi.

Naipongeza Serikali ya Dk. Magufuli kwa kufanikisha upatikanaji wa ujenzi huu wa bomba la mafuta kutoka Uganda. Haikuwa kazi rahisi Tanzania kupata fursa hii ya bomba la mafuta kutoka nchini Uganda kutokana na ushindani mkubwa uliokuwepo.

Narudia tena kumpongeza Dk. Magufuli kwa kutuletea mradi huu wa bomba la mafuta utakaokuwa na tija kwa Taifa vizazi na vizazi. Ni jukumu letu Watanzania kuulinda mradi huu wa bomba la mafuta.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Dk. Magufuli

Na Emmanuel J. Shilatu
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top