Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Breaking news .... Madiwani 3 Chadema waachia ngazi

MADIWANI  watatu  wa  chama  cha  Demokrasia na maendeleo  (CHADEMA)   jimbo la  Iringa mjini   wamemwandikia barua  msimamizi wa  uchaguzi  jimbo la  Iringa mjini kujiuzulu  nafasi  zao kuanzia leo  Augosti  23 majira ya saa40  jioni
Wakizungumzia  azma   hiyo ya  kujiuzulu nafasi  zao  madiwani  hao Baraka Kimata  wa  kata ya  Kitwiru  na  madiwani  wenzake  wawili  wa viti maalum Leah Mlelewa  na  Husna Ngasi  walisema   kuwa  wamefikia  uamuzi huo baada ya  kuchoshwa na  mwenendo wa  chama  hicho  jimbo la  Iringa mjini na  hivyo  wameamua  kuachia nafasi zao na  kubaki bila  kuwa  wanachama ama  viongozi  wa  chama   hicho.

Kimata  ambae alikuwa ni katibu mwenezi wa chadema   jimbo la  Iringa mjini na  mwenyekiti  wa madiwani jimbo la  Iringa mjini  alisema nafasi  zake  zote  ameziacha na  kuwa  kwa  sasa ataendelea na  shughuli  zake nyingine  nje  ya  siasa  kwani  siasa  kwa ujumla wake  imemshinda .


Kwani  alisema  pamoja na  kuwa chama  chao  ni  chama cha  Demokrasia  ila  katika  jimbo la Iringa mjini  Demokrasia  imekuwa  ikivurugwa na  baadhi ya  viongozi  na  hata  kupelekea  madiwani  kuona  chama  hichop  ni  kichungu na  hivyo hatua yao ya  kujiuzulu  ni kilelelezo tosha  kuwa  ndani ya  chama  hicho  Iringa mjini  hakuna  usalama.

Alisema  mbali ya  sababu  nyingine   zilizopelekea  kujiuzulu  kwake na  wenzake  ila  bado  amekuwa  akikosa  ushirikiano  kutoka kwa  mbunge  wa  jimbo mchungaji  Peter Msigwa  ambae  toka  amechaguliwa  kata  yake  hajapata  kufanya  ziara ya  aina  yeyote  na  hivyop   kutokana na kubaguliwa   huko na  pamoja na  kuendelea  kudidimizwa   haki  yake wakati wa  kuwania nafasi mbali mbali  ikiwemo ya   umeya na unaibu  meya ameona  ni vema  kutojihusisha na  masula la  siasa .

"  kumekuwepo na  maneno  kutokana kwa  watu  kuwa   tumenunuliwa  kwa ila  ukweli  utabaki pale pale  tumeondoka kwa  kukwepa  demokrasia  mbaya ndani ya  chama   chetu na  tutakuwa   huru  kujiunga na  chama  chochote kama  ACT  Wazalendo ama  chama  kingine  chochote  chenye Demokrasia  nzuri "


Kwa  upande wake  Mlelewa  ambae  alikuwa ni afisa  habari  wa  jimbo la Iringa mjini na katibu  wa baraza la  vijana  la  Chadema (BAVICHA ) na katibu wa madiwani alisema  ameachia  ngazi  nafasi  zote  ikiwemo  ya  udiwani  kama  wenzake na  sababu  za kufanya  hivyo ni  ubabe  ndani ya  chama  hicho .

Husna  Ngasi  alisema  pamoja na  sababu nyingine  ameachia  ngazi  kutokana na  kubaguliwa kwa  misingi ya itikadi  zake  za  dini  na  kuwa kwa muda amekuwa akinyanyapaliwa na  hivyo  kuamua  kukaa  pembeni .

Kwa  upande wake  msimamizi  wa  uchaguzi   jimbo la  Iringa mjini  Dkt Wiliam Mfere alipoulizwa na mwandishi  wa matukiodaimaBlog  kwa  njia ya  simu jana   jioni alisema  kuwa  bado hajapokea  barua  ya  kujiuzulu kwao  kwani hakuwepo  ofisini na kuwa akipatatazitolea maelezo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top