Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kauli ya Chadema kuhusu kuzuiwa kufanya Kongamano Geita

CHADEMA walikutana na Waandishi wa Habari na kutoa tamko lao baada ya kuzuiwa na Jeshi la Polisi Geita kufanya Kongamano kumuenzi aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo.

Akizungumza baada ya zuio hilo mmoja wa wanachama wa CHADEMA, Dr. Mussa Mdede ambaye alikuwa mmoja wa watoa mada katika Kongamano hilo, alisema kitendo cha Polisi kuzuia Kongamano hilo ni kukiuka sheria.

>>>”Kongamano ambalo limezuiwa ni shughuli ya ndani ambayo kimsingi Sheria ya Vyama vya Siasa inatulinda. Kimsingi ni Kongamano ambalo lilikuwa halali na tunapofanya Kongamano la ndani hatuhitaji ulinzi wa Jeshi la Polisi.

“Jeshi la Polisi linahitajika kuimarisha ulinzi na usalama kwenye mikutano ya hadhara, ndivyo Sheria Namba 5 ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 1995 inavyosema, si vinginevyo. Kitu ambacho wamekifanya kipo kunyume na Sheria.”

Aidha, Mdede amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kuwakumbusha Askari Polisi majukumu yao kwa kuwa siku za hivi karibuni wanatumika kisiasa.

“CHADEMA tunasema, kwanza tunamwambia IGP Simon Sirro kwamba awakumbushe Askari wake wafanye kazi kwa weledi wasifanye kazi kwa kisiasa. Katika Awamu ya Tano Jeshi la Polisi limekuwa likifanya siasa waziwazi.” – Mussa Mdede.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top