Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mbunge akesha akiulilia Ubunge


Image result for tears

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 

Katibu Mkuu wa cuf aliyesimamishwa Maalim Seif Sharif Hamad jana amelazimika kuongozana na ustaadhi mmoja kwenda nyumbani kumfariji mmoja kati ya wabunge  wa viti maalum Khadija Salum "Makontena" aliyefukuzwa uanachama na kupoteza ubunge huku akilia kutwa kucha .

Habari za uhakika  na uthibitisho wa kuwepo  video,  inamuonyeaha Maalim seif akiwa ukumbini mwa nyumbani kwa mbunge huyo wa zamani huku ustaadhi mmoja akisoma utenzi wa huzuni ili kumpa maliwazo, nasaha na faraja. 

Chanzo chetu kimoja ndani  kimeeleza kuwa Khadija ameangusha kilio mara baada ya kupata habari  mahakama imeamua kisheria yeye na wenzake na wabunge kwa wahunge viti maalum upande wa Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba. 

Maalim seif akifuatana na mmoja wa wanasiasa nguli Mwakilishi wa zamani wa jimbo la mji mkongwe Ismail Jussa ladhu, wanaonekana kwenye video hiyo huku mbunge huyo akilia kwa uchungu kufuatia kupoteza ubunge wake . 

Simu ya Jussa mara kadhaa imekuwa ikiita bila kupokewa na hata alipotumiwa ujumbe wa maneno hakuonyesha ushirikiano .

Jamaa wa karibu wa mbunge huyo  (jina tunalo) akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake amesema mbunge huyo toka apate taarifa za kupoteza kiti amekuwa akilia huku alimtupia lawama Maalim seif kwa kukataa kufanya mazungumzo ya upatanishi na Mwenyekiti wao Profesa Lipumba. 

"Shangazi kilio chake anamshutumusana  Maalim seif kwa kusinabisha avuliwe ubunge,maisha ni magumu pia malengo yake yote yamekwama huku mwenzao kila mwezi akipokea marupurupu ya fedha za Waziri Kiongozi na Makamu wa keanza wa Rais mstaafu zanzibar  "Kikieleza chanzo hicho. 

Aidha alisema Mbunge huyo amekuwa akilaumu tabia ya viongozi wa cuf kuwaambia wanachama maneno ya uongo kwanba Rais  wa zanziabr Dk Ali Mohamed Shein ataondolewa madarakani na Maalim Seif kuwa Rais mpya jambo ambalo si kweli. 

Taarifa zaidi zinaeleza  tokea uamuzi wa mahakama upite kisheria na wabunge nane kuvuliwa nyadhifa zao huku Rita ikiitambua bodi ya wadhamini upande wa Mwenyekiti na Tume yaTaifa ya uchaguzi kupeleka maji mapya bungeni ,mijadala ya siasa imevia na baadhi ya wafuasi wa cuf hawataki kumsikiza Maalim seif. 

Ali Sultan Mmanga anayeishi kikwajuni alisema ubishi na kushauriwa vibaya kwa katibu mkuu  na wanasiasa wapambe waliohamia cuf toka ccm kumekifikisha chama hicho mahali pagumu na hatma yake sasa haitabiriki. 

Mmanga alisema pirika na ingia toka za wapambe kabla na baada uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 zilionyesha wazi Maalim Seif angepelekewa puta na ushauri wao ambapo  sasa wamekiacha chama hicho na kufanya shughuli zao binafsi.  

"Sikupenda kabisa urafiki wa ghafla kati ya Maalim seif na Rais mstaafu Dk Amani Karume , Edy Riyami au Mansoor Yussuf Himid, hawakuwa na nia njema kwake,wale wazazi  wao ni wana mapinduzi halisi na katu  hawawezi kubadili misimamo yao kama ilivyotarajiwa"Alieleza mwanacuf huyo. 

Mwachama huyo alisema tokea mwaka 1995 Riyami alikuwa ndiye mshirika wa mkonO wa kuume wa Rais mstaafu Dk salmin Amour katika mipango yote ya kampeni ambapi Mansoor akimsaidia kwa nguvubzake zote shemeji yake Dk Karume tokea mwaka 2000 hadi akiondoka madarakani mwaka 2010. 

End
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top