Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mwalimu mbaroni kwa kufanya mapenzi na mwanafunzi wakeMwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Igurubi, Maganga Ngassa (35) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari kidato cha nne, Kata ya Mwisi wilayani hapa.

Mwendesha Mashitaka wa Polisi Igunga, Elimajid Kweyamba alidai mbele ya Hakimu Juhudi Mdonya, kwamba Julai 25, mwaka huu saa 9 alasiri katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Forest au Chacha iliyoko Mtaa wa Mwayunge mjini Igunga, kinyume na sheria za nchi, Ngassa alifanya mapenzi na mwanafunzi  mwenye umri wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari iliyoko Kata ya Mwisi kidato cha nne (jina linahifadhiwa).

Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 18, mwaka huu itakapotajwa tena.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top