Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Nafasi za kazi mpya toka Serikali


Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam anawatangazia wananchi wote wenye sifa za kuajiriwa kuleta maombi yao ya kazi kwa nafasi zifuatazo:
 
1.0 KATIBU MAHSUSI III (PERSONAL SECRETARY III)-NAFASI (2) -NGAZI VA MSHAHARA TGS.B
 
SIFA ZA KUAJIRIWA:
Waombaji wawe na Elimu ya Kidato cha Nne/Sita waliohitimu mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua yaTatu.

Wawe wamefaulu somo la Hati Mkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno (80) kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika Programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
 
KAZI ZA KUFANYA:
(i)    Kuchapa barua na nyaraka za kawaida.
(ii)    Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekezniehemu wanapoweza kushughulikiwa.    s    -
(iii)    Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au kituellochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
(iv)    Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maafisa walio katika sehemu alipo na kuyakusanya, kuyatunza na kurudisha sehemu zinazohusika.
(v)    Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, mladi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi na kumwarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
 
2.0 MWENDESHA MITAMBO II (PLANT OPERATOR II)- NAFASA (2) - NGAZI YA MSHAHARA - TGOS A

SIFA ZA KUAJIRIWA:
Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha nne ambaye ana leseni daraja la G ya kuendesha mitambo na ujuzi wa kutunza vyombo vya aina hiyo, ujuzi sio chini ya saa 300 (miezi mitatu 3) bila kusababisha ajali

KAZI ZA KUFANYA:   
Kuendesha Mitambo chini ya usimamizi wa Dereva wa Mitambo mwenye uzoefu.
 
3.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II (RECORDS MANAGEMENT ASSISTANT II) - NAFASI (1) - NGAZI YA MSHAHARA TGS.B

SIFA ZA KUAJIRIWA:   
Waombaji wawe na elimu ya kidato  cha Nne/Sita wenye Cheti cha Utunzaji wa kumbukumbu wa fani ya Masjala

KAZI ZA KUFANYA:
(i)    Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
(ii)    Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
(iii)    Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi na somo.
(iv)    Kuwekekupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki katika masjala.
(v)    Kuweka kumbukumbu; barua, nyaraka nk katika mafaili.
(vi)    Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
 
4.0 MASHARTI YA JUMLA:
(i)    Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa kuanzia miaka 18 usiozidi miaka 45.
(ii)    Waombaji wote waambatishe nakala ya Vyeti vya Taaluma, Vyeti vya Kidato cha Nne na Sita, Cheti cha Kuzaliwa, picha mbili (2) passport size ya hivi karibuni iandikwe majina ya mwombaji kwa nyuma.
(iii)    Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono na mwombaji mwenye zikiambatishwa na maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika na majina ya wadhamini watatu (referees) wa kuaminika na namba zao za simu.
(iv)    Testimonials na Provisional Results", Statement of Results, hati matokeo za kidato cha nne (Form IV or VI results slips HAVITAKUBALIWA,
(v)    Waombaji waliosoma Nje ya Nchi wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA)
(vi)    Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza.
(vii)    Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
(viii)Tangazo hili pia linapatikana kwenye Tovuti ya Jiji www.dcc.go.tz
(ix)    Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 Agosti, 2017.
(x)    Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika Ofisi za Jiji HAURUHUSIWI, MAOMBI VOTE YATUMWE KWA NJIA YA POSTA.
 
5.0 MAOMBI YATUMWE KWA:
 
Mkurugenzi wa Jiji, 
Halmashauri ya Jiji,
 "Ukumbi wa Jiji"
S.L.P. 9084,
1 Barabara ya Morogoro, 
11882 DAR ES SALAAM
 
6.0 Waombaji waliokidhi sifa wataarifiwa tarehe ya kufanya usaili kwa njia ya maandishi kupitia magazeti yaliyotumika kutangaza nafasi hizi pamoja na simu za mikononi au Tovuti: www.dcc.go.tz
 
Waziri Kombo
KAIMU MKURUGENZI WA JIJI,
HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

Source: Daily News, Wednesday, August 2, 2017
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top