Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC Makonda ashusha neema mpyaaa




NEEMA KWA WENYE UHITAJI WA MIGUU BANDIA.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda amefanikiwa kupata MIGUU YA BANDIA ya Kuhudumia wananchi MIA MBILI (200) itakayoweza kuwasaidia wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wenye mahitaji.

Miguu hiyo yenye thamani ya Shilingi Milion 600 hadi bilioni 1.2 ENDAPO watu wote 200 watahitaji miguu yote miliwi itatolewa bila BILA MALIPO (bure) kwa wananchi waliopata ajali na kushimdwa kupata miguu hiyo kutokana na kushindwa KUMUDU gharama za kununua miguu hiyo ambapo kwa MGUU mmoja unagharimu Milion TATU (3,000,000)

Mhe MAKONDA amewataka wananchi WOTE wenye UHITAJI wa miguu ya BANDIA NA ambao hawana UWEZO wa kumudu GHARAMA kufika ofisini ya mkuu wa mkoa siku ya Jumatatu Tarehe 14/08/2017 na Jumanne Tarehe 15/08/2017 kwaajili kukutana na wataalamu wa miguu watakaochukua VIPIMO kwaajili ya kutengenezewa miguu kulingana na maumbile yao.

"Nimepewa kazi ya MKOA kuhudumia MAKUNDI yote, nafahamu kwenye mkoa wangu wapo waliopata ajali na wengine wakavunjika miguu lakini PESA ya kupata miguu ya BANDIA ili waachane na magongo kwao imekuwa ni moja ya CHANGAMOTO, kutokana na sababu hiyo nimeona vyema nifikiri namna ya KUWASAIDIA wananchi ambao hawana UWEZO ili waweze kupata, nimefanikiwa kupata wadau watakaonipatia miguu ya kuhudumia wananchi 200" Nahii ni awamu ya kwanza ,Alisema Makonda.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
10/08/2017
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top