Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Zitto Kabwe akamatwa na polisi Akiwa Uwanja wa Ndege Dar

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amekamatwa na jeshi la polisi usiku huu katika uwanja wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam akitokea Kigoma.

Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis amethibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo wa chama chake na kusema kuwa kwa sasa wanasheria wa chama hicho wanafuatilia kujua sababu ya kiongozi wa chama chao kukamatwa na jeshi la polisi.

"Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi muda huu uwanja wa ndege wa JNIA, Dar es salaam wakati akitoka Kigoma. Kwa sasa wanasheria wa chama wanafuatilia kujua sababu za kukamatwa kwake" alisema Abdallah Khamis

Asubuhi ya leo kulikuwa na taarifa kuwa Katibu wa Bunge Dkt. Thomas kashililah alitoa amri kwa jeshi la polisi kumkamata Mbunge huyo wa Kigoma Mjini na kutakiwa kumfikisha mjini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kauli ambazo amewahi kuzitoa juu ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Job Ndugai pamoja na Bunge lenyewe.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top