Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Nyalandu avaa gwanda rasmi

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu, Jijini Mwanza katika uwanja wa Shule ya Msingi Mhandu kwenye kampeni ya kumnadi mgombea udiwani Godfrey Mahame.

"Nimeisubiri kwa shauku kubwa siku hii ya leo ili nipate fursa ya kupigania mageuzi ya kisiasa na ya kiuchumi Tanzania," amesema Nyalandu baada ya kukabidhiwa kadi.

Amesema ana shauku, furaha na heshima kukaribishwa rasmi kuwa mwanachama wa Chadema. Nyalandu ameongeza kuwa katika majira na nyakati ambazo Taifa linapitia, mabadiliko ya kisiasa nchini Tanzania ni lazima.

"Naungana na chama hiki pendwa ili tutembee pamoja mtaa kwa mtaa kijiji kwa kijiji tuwaambie wananchi wakati wa ukombozi ni sasa," alisema Nyalandu.

"Saa ya mabadiliko imefika kwa mtu yeyote miongoni mwetu, tumepewa utayari wa kubadilisha mwelekeo wa nchi," amesema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top