Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CCM HAKUNA SABABU YA KUFANYA KAMPENI 2020 TUNAHITAJI KUPITA BILA KUPINGWA: KHERI JAMES

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal

Wajumbe wa Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018. 

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James (Kulia) akieleza umuhimu wa wakazi wa Kata ya Kimandolu kumchagua Ndg Gaudence Limona kuwa diwani wao wakati akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018.
 Kikao kikiendelea
Wajumbe wa Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu, Leo 12 Januari 2018. 


Na Mathias Canal, Arusha

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndg Kheri Denice James amesema kuwa CCM haina sababu ya kufanya kampeni katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 badala yake kuna kila sababu ya kupita bila kupingwa kutokana na uimara wa CCM na serikali yake.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa ameyasema hayo Leo 12 Januari 2018 wakati akizungumza na Timu mbalimbali za kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kimandolu Mkoani Arusha kutoka jumuiya za CCM sambamba na mabalozi wote wakati wa kikao cha ndani kilichofanyika Mtaa wa Kijenge Kaskazini Kata ya Kimandolu.

Kheri alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kutatua kero zote zisizo rafiki kwa wananchi kwa utekelezaji wa Mkataba wa wananchi na CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.

Kheri aliwataka wananchi kujitokeza kwa mwingi kupiga kura hapo kesho 13 Januari 2018 kwani ni haki yao ya msingi kikatiba lakini pia aliwakumbusha kuwa katika uchaguzi huo wananchi wanapaswa kumchagua Diwani wa CCM kwa ajili ya maendeleo endelevu kwa ajili ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake.

Katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika kesho katika Kata ya Kimandolu Ndg Gaudence Limo ndiye mgombea wa CCM ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Arusha.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Kheri alivifananisha vyama vya upinzania nchini Tanzania na waharamia ambao kazi yao kubwa ni wizi na ujambazi, ujangili, udokozi, utapeli na uongo hivyo kupitia ulaghai wao haviwezi kufanikiwa kushika dola kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Aliwasihi vijana kukumbuka majukumu yao kama nguvu kazi ya Taifa kuwa ni pamoja na kusema ukweli, kuwajibika na kuwa watendaji na viongozi madhubuti sio viongozi biskuti.

Aidha, Kheri amewafikishia wakazi wa Arusha salamu za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuwa anahitaji ushindi wa kishindo wa zaidi ya kura 12,000 na hiyo itakuwa zawadi pekee kwake.

“Ndugu zangu sisi wana CCM tunaweza kujadiliana harusi itafungwa vipi na wapi, tunaweza tukajadiliana aina ya magari ya kununua lakini hatuwezi kuwa na mjadala wa namna yoyote ile kwenye utafutaji wa dola ni lazima CCM ishinde” Alikaririwa Kheri

MWISHO
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top