Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Kheri James awasili rasmi ofisini

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kheri D James akisalimiana na Mtumishi wa Makao Makuu ya Umoja wa Vijana  wa CCM Bi.Sheila Alipowasili katika Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Umoja wa Vijana Wa CCM Upanga Leo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana(UVCCM) Taifa Ndg.Shaka Hamdu Shaka (kwanza kushoto)akimtambulisha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri D James kwa Makatibu wasaidizi wakuu alipowasili ofisi ndogo za UVCCM Upanga leo.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) Ndg.Shaka Hamdu Shaka akimuonyesha Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri D James moja ya Ofisi ya Makao makuu.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg.Kheri D James akisaini kitabu Rasmi Kuingia Ofisini Leo Makao makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM Upanga.
 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Bi Thabia Mwita akisaini kitabu,.
 Viongozi wakuu wakiwa katika Ofisi ya Mwenyekiti Wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Ndg. Kheri D James akizungumza na Watumishi wa Makao Makuu ya UVCCM Upanga leo.

*"NINATAKA MUWE NA UADILIFU, UTII, UTUMISHI, UBUNIFU NA NIDHAMU" - KHERI JAMES*

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Ndugu Kheri James amesisitiza juu ya mambo anayoyataka  Watumishi, Maafisa na Wanachama wazingatie utii, uadilifu,utumishi, ubunifu na nidhamu katika kipindi cha uongozi wake.

Hayo yamesemwa na Kheri James wakati Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mpainduzi (UVCCM) Taifa alipowasili rasmi Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya UVCCM Upanga Jijini Dar Es Salaam leo Jumatatu Januari 15, 2018.

Kheri James alipokelewa mapema leo asubuhi na Makamu Mwenyekiti UVCCM Taifa Ndugu Tabia Maulid Mwita na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Ndugu Shaka H. Shaka ambaye alimtembeza kwenye Ofisi za Idara mbalimbali na kupata fursa ya kutambulishwa na kuwafahamu Watumishi na Maafisa mbalimbali wa Ofisi Ndogo Makao makuu UVCCM.

Kheri ambaye alipata pia fursa ya kuzungumza na Wakuu wa idara pamoja na Watumishi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu UVCCM na kuwaambia kuzingatia nidhamu, utumishi, utii na ubunifu ili kujenga jumuiya mpya na imara ya UVCCM.

"Ninataka Watumishi muwe na heshima na nidhamu kwa Watu wote. Muwe watiifu na wabunifu kwenye utendaji kazi wenu" alisema Kheri.

Kheri alisisitiza Watumishi kuepuka matabaka, makundi, maneno maneno na badala yake waongeze upendo na yeye kama Mwenyekiti hayupo tayari kusikiliza maneno ya mitaani anachotaka ni Watu wafanye kazi, watimize wajibu wao.

"Kwa muda mfupi nimesikia maneno mengi  mabaya yanayowahusu na ningekuwa Mwenyekiti ninayesikiliza maneno ya barabarani hakuna ambaye angebaki salama. Kikubwa naomba tufanye kazi, tuwe wabunifu na tuepuke maneno maneno. Usalama wa Mtu upo kwenye kufanya kazi." alisema Kheri.

Aidha Mwenyekiti huyo wa UVCCM, Ndugu Kheri James alisisitiza kujenga mahusiano na ngazi za chini na ameandaa utaratibu wa kila wiki kukutana na Wanachama pamoja na viongozi.

"Nimeamua kutenga kila siku ya Jumanne kukutana na Wanachama wa UVCCM wenye kero mbalimbali na kila siku ya Alhamis kukutana na viongozi mbalimbali." alisema Kheri.

Kheri alizidi kusisitiza, "Kila Mwanachama anayekuja kuniona ahakikishe suala lake ameshaliwakilisha ngazi za chini za Tawi, Kata, Wilaya na Mkoa. Na pia Makatibu wa Mikoa na Wilaya wawe na ushirikiano kwa kuwasilisha taarifa zinazohusu vijana kwenye ngazi husika ya Serikali."

Kheri amesisitiza Vijana kote nchini kuelewa kauli mbiu yake ya *Tukutane Kazini* imelenga Vijana, Wanachama na Watumishi wote kuamka na kutimiza wajibu wao kwa jumuiya na Chama ili kujenga jumuiya imara itakayoendelea kuwa tegemeo na mkombozi wa CCM na Serikali.

Imetolewa na:

Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi
UVCCM TAIFA.

15/01/2018


Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top