Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Benki Zawahakikishia Wafanyabiashara Mikopo....Ni Wale Wanaotaka Kununua Pamba

BENKI mbalimbali nchini zimewahakikishia wafanyabiashara wa zao la pamba kuwa zina fedha za kutosha kuweza kuwakopesha ili wanunue pamba yote itakayozalishwa katika msimu wa mwaka huu nchini.
 
Pia viongozi wa benki hizo wamesema wako tayari kusaidia katika uwekezaji wa miundombinu ya aina yeyote ama eneo litakalohitaji mkopo wa fedha ili kufanikisha mchakato wa ununuzi wa pamba katika msimu huu ikiwa ni pamoja na kusaidia ujenzi wa maghala.
 
Hayo yamesemwa jana  (Jumatano, Februari 21, 2018) na viongozi wa benki mbalimbali nchini katika mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa uliowahusisha wafanyabiashara wote wa pamba , Wakuu wa Mikoa ,Viongozi wa Halmashauri na wadau wote.
 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa benki za NMB, CRDB, TIB, EXIM, AZANIA, Mkombozi, Bank of Africa, Equity na Eco waliwahakikishia wafanyabiasha hao mbele ya Waziri Mkuu kwamba wana fedha za kutosha na wako tayari kuwapa mikopo ili wakanunue pamba mara msimu utakapoanza.
 
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Mkuu amewataka wanunuzi wa zao hilo kuandikisha katika ofisi ya Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba kiasi cha pamba wanachohitaji kununua pamoja na maeneo ambayo wanatamani kwenda kununua.
 
Waziri Mkuu amesema suala hilo litaiwezesha bodi kufahamu idadi ya wafanyabiashara watakaonunua pamba pamoja na kiasi wanachohitaji na eneo husika. “Serikali itaendelea kusimamia zao hilo kikamilifu.”

Amesema kwa sasa wanauhakika kuwa pamba yote itanunuliwa kwa sababu benki zimewathibitishia kwamba ziko tayari kuwakopesha wafanyabiasha, hivyo wadau wote watambue kuwa Serikali itashirikiana nao hadi katika hatua za mwisho za ununuzi.

Waziri Mkuu aliwahakikishia wafanyabiashara hao kwamba maombi waliyoyatoa kuhusu uboreshaji wa mauzo ya zao hilo yatayafanyiwa kazi na Serikali itaendelea kusimamia zao hilo ili ununuzi wake uwe rahisi.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba amesema wamejipanga kikamilifu katika kudhibiti ubora wa pamba, ambapo amewataka viongozi wa maghala wasipokee pamba chafu.

Pia amewataka wakulima wa pamba wasithubutu kuchanganya na maji, mawe au mchanga kwa sababu wataharibu soko. Serikali itapambana na watu wote wakaothubutu kuharibu zao hilo kwa kcuhukua hatua kali za kisheria kwani huo ni uhujumu uchumi.

Aliendelea kusema kuwa uamuzi wa Serikali kusimamia ongezeko la uzalishaji wa zao la pamba unakwenda sambamba na mazao mengine makuu ya biashara ambayo ni korosho, chai, tumbaku, kahawa na mahindi kwa upande wa chakula.

Dkt. Tizeba amesema inatazamiwa kuwa ifikapo 2021 mchango wa mazao katika pato la Taifa unakadiriwa kufikia sh. trilioni 13.6, ambapo yataliwezesha Taifa kuvuka mstari wa kiwango cha umasikini.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa zao la pamba lina mchango mkubwa katika kukuza uchumi, hivyo watahakikisha zao hilo linaendelea kukua.

Dkt. Mpango amezitaka benki zichukue tahadhari kwa mikopo chechefu  hivyo wajiridhishe kama wakopaji wote wanatumia mikopo hiyo kwa mujibu wa makusudio.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 21, 2018.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top