Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mvua za Masika zinatarajiwa kuanza mwezi Machi maeneo mengi hapa nchini



Dar es Salaam. Mvua za wastani mpaka juu ya wastani zinatarajiwa kuanza kunyesha katika kipindi cha wiki ya kwanza ya mwezi Machi hadi Mei mwaka huu katika maeneo mengi hapa nchini.

Hayo yameelezwa leo Februari 15, 2018 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk Agnes Kijazi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mwelekeo wa mvua katika kipindi cha msimu wa masika.

Amesema zinatarajia kuleta athari katika sekta mbalimbali kutokana na vipindi vifupi vya mvua kubwa vinavyoweza kusababisha mafuriko

Dk Kijazi ametoa ushauri kwa sekta mbalimbali kuchukua tahadhari na kujiandaa ili kutumia vyema utabiri huo hasa menejimenti za maafa.

Amesema ukanda wa Pwani ya Kaskazini ikiwemo mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza ya Machi.

“Mvua hizi zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo hayo na Kusini mwa Mkoa wa Tanga, maeneo yaliyosalia yaliyo Kaskazini mwa Mkoa wa Tanzania yanatarajiwa kupata mvua za chini ya wastani,” amesema Dk Kijazi.

  1. Aidha, Dk Kijazi ameshauri wananchi kutumia kipindi hiki kuhakikisha wanafanya kilimo na usalama wa chakula, mifugo na wanayamapori.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top