Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri Mkuu: Shida Ya Maji Jiji La Mwanza Kuwa Historia....Ni Baada Ya Serikali Kuanza Ujenzi Wa Miradi Ya Sh. Bil. 112

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipokea mabomba ya maji yenye urefu wa kilomita tano kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Mwanza Plastics, Joel Makanyaga wakati alipotembelea kiwanda hicho jijini Mwanza , Februari 20, 2018. Kulia ni Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina mabulla. Mabomba hayo yatatumika kupeleka maji katika Kituo cha Afya cha Karume kilichopo kata ya Bugogwa wilayani Ilemela.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


CCHANGAMOTO ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Jiji la Mwanza kuwa historia baada ya Serikali kuanza utekelezaji wa ujenzi wa miradi mikubwa miwili ya maji yenye thamani ya sh. bilioni 112.

Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (Jumanne, Februari 20, 2018) wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Halmashauri za Jiji la Mwanza, Ilemela na Nyamagana akiwa katika siku ya sita  ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.

Waziri Mkuu amesema miradi hiyo inahusisha kuboresha upatikanaji wa maji katika maeneo ya pembezoni wenye thamani ya sh. bilioni 75 ambao utahusisha ujenzi wa chanzo kipya cha maji kwenye eneo la Butimba chenye uwezo wa kutoa lita milioni 40 kwa siku.

Ametaja maeneo yatakayonufaika na mradi huo kuwa ni Butimba, Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Sawa, Lwanhima, Kishiri, Nyahingi, Luchelele, Malimbe, Bulale, Fumagila, Usagara, Kisesa, Buswelu, Nyamwilolelwa, Kahama, Nyamadoke, Nyamhongolo, Mondo, Kiseke, Kangae, Meko, Nsumba na Bulola.

Waziri Mkuu amesema mradi mwingine ni wa kuboresha upatikanaji wa maji katika maeneo ya milimani wenye thamani ya sh. bilioni 37 ambao ulianza kutekelezwa Februari, 2017 na unatarajiwa kukamilika Agosti 2018.

Amesema wakazi 105,649 wanaoishi katika maeneo ya milimani hususan yaliyo juu ya matenki ya maji ambayo hayapati huduma kwa sasa watanufaika. Maeneo hayo ni Nyasaka, Bugarika, Nyegezi, Capripoint, Mjimwema, Nyakabungo na Kitangiri.

Amesema Serikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini watapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka viongozi na watendaji wa Jiji la Mwanza kuhakikisha wanashirikiana katika kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi wa dini, kabila wala kipato. Pia amewataka watambue miiko na ukomo wa madaraka yao.

Amesema watumishi hao wanatakiwa wawe waaminifu na wasimamie vizuri matumizi ya fedha za uetekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye maeneo yao na wahakikishe zinatumika katika miradi husika kama ilivyoelekezwa na Serikali.

Pia Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Bw. Kiomoni Kibamba kuifuta Taasisi ya Bunge la Jamii kwa sababu inakiuka sharia na kazi inazofanya zinalingana na za bunge. Taasisi hiyo ilisajiliwa na ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 20, 2018.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top