Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HAKIKA, DK. MAGUFULI NI RAIS WA WANYONGE



*Hakika, Dk. Magufuli ni Rais wa Wanyonge*

*Na Emmanuel J. Shilatu*

1. Serikali yake inatoa ELIMU BURE kuanzia Elimu ya Msingi mpaka Sekondari. Hii imesaidia sana Watoto wa Wanyonge kupata haki ya elimu, kupata haki ya kuelimika.

2. Aliondoa ofisi na kuamuru zigeuzwe kuwa wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Muhimbili. Leo hii akina Mama hawajifungulii tena chini bali kitandani, leo hii akina Mama hawalali wawili wawili bali kila kitanda na Mtu mmoja.

3. Aliamuru wakazi wa Pwani wapewe hekari 65 kutoka katika ardhi ya Magereza. Hii ilisaidia zoezi la wakazi hao kuondolewa lisitishwe mara moja na mpaka kesho Watu wanaishi kwa amani tele katika eneo hilo.

4. Aliamuru Wamachinga na Mama Lishe kutokusumbuliwa na kamata kamata ya Mgambo. Leo hii Wamachinga wanafanya shughuli zao kwa uhuru mkubwa.

5. Anahakikisha Wazee wanapewa Bima za Afya za Matibabu bure. Tangu Serikali ya awamu ya 5 yake Dk. Magufuli iingie madarakani kasi ya utoaji wa Bima za afya kwa Wazee zaidi ya miaka 60 wasiojiweza imeongezeka. Hii imesaidia afya za Wazee wetu kuwa na uhakika wa usalama zaidi.

6. Amehakikisha kila Hospitali ya Serikali inajengewa duka la dawa ndani kupitia MSD. Hii imesaidia upatikanaji wa dawa muhimu na kwa bei nafuu ambazo kila Mtu atamudu. Wanyonge hawateseki tena kwa kukosa dawa ama kulanguliwa dawa kwa bei kubwa.

7. Amehakikisha rasilimali za Taifa mfano madini, mchanga ama Wanyama hai kutokusafirishwa nje. Hii imesaidia rasilimali  za Taifa kuweza kuwanufaisha Watu wote wakiwemo wanyonge.

8. Ameimarisha hali ya uwajibikaji na uadilifu kwa Watumishi wa umma. Hii imesaidia uimarishwaji wa utendaji kazi na utolewaji wa huduma kwa haraka na kwa Watu wote. Leo hii Watu wa hali ya chini wanapata haki sawa ya kusikilizwa na kuhudumiwa sawa na wanaojiweza tofauti na hali ya awali ilivyokuwa si ya kuridhisha.

9. Baadhi ya Watoto wa maskini waliokuwa wakisota mitaani kwa kukosa ajira wamepata fursa za ajira rasmi mara baada ya kufanikiwa kuwatimua wenye vyeti feki ambao hawakustahili kuwepo kwenye nafasi walizokuwa wakizitumikia.

10. Alifuta kodi ya usafirishaji wa mazao kwa Wakulima wanaosafirisha mazao yao chini ya tani moja.

11. Anawasikiliza na kutatua kero pale pale za Watu wanaokimbilia kwake wakati wa mikutano ya hadhara. Watu hawa wengi wao ni wanyonge walioshindwa kupambana na wenye mabavu ya fedha na hadhi.

12. Anahakikisha Watanzania wanapatiwa kipaumbele cha ajira kwenye miradi yote mikubwa ya Kiserikali ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta, ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge.

13. Serikali yake imeamuru kila Mwajiri kutoa mkataba wa ajira Watumishi wake waliifanya kazi ya kibarua kwa zaidi ya miezi sita pasipo kuajiriwa.

14. Anatoa magari ya wagonjwa (Amburance) kwa Wabunge mbalimbali wakapeleke kwenye majimbo yao zikasaidie Watu wanyonge kwenye maeneo yao.

15. Aliamuru Wafanyabiashara wa Kigoma Mjini wasilipishwe kodi ya vibanda ya Tsh. 50,000/= na badala yake walipe Tsh. 15,000/=.

Matendo haya yote na mengineyo yanatoa picha ya namna Rais Magufuli alivyoamua kuwa upande wa Watu wanyonge. ... Sisi Wananchi wa Tabaka la chini tunamwelewa sana Rais Dk. Magufuli.

*Tutaendelea Kumuunga Mkono Rais Magufuli*

*Shilatu E.J*
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top